Siku kadhaa tangu kutangazwa kukamatwa kwa mwanamuziki wa nchini Uganda, Iryn Namubiru huko Japan kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya, ufafanuzi zaidi juu ya tukio hili umetoka na kufahamika kuwa, alichokamatwa nacho mwanamuziki huyu ni unga wa ndizi maarufu kama matoke ambao alikuwa amebeba kuwapelekea wenyeji wake Japan.
Imefahamika kuwa, msanii huyu pia alitiliwa shaka zaidi kutokana na kuwa raia wa Uganda ambaye pia ana passport ya Ufaransa, kitu ambacho kiliwaongezea wasiwasi maafisa usalama wa uwanja wa ndege wa Japan.
Hadi sasa inataarifiwa kuwa msanii huyu yupo bado chini ya ulinzi na kesi hii aliyoipata inahatarisha uwezekano wa yeye kushinda kesi ya malezi ya mtoto ambaye kwa sasa wanamgombania na mme wake, raia wa Ufaransa ambaye kwa sasa wametengana.