Wednesday, 8 May 2013

OMG!!!!! CHRISTIANO RONALDO AMEFIKISHA MAGOLI 200 KATIKA MECHI 197 ZA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO

KLABU ya Real Madrid imeendelea kuifanya Barcelona isubiri kutangaza taji la 22 la ubingwa wa La Liga angalau hadi Jumapili baada ya Cristiano Ronaldo kufunga bao lake la 200 katika ushindi wa 6-2 nyumbani dhidi ya Malaga iliyomaliza na wachezaji tisa usiku wa Jumatano.
 
Barca inahitaji pointi mbili zaidi kujihahakishia ubingwa wa nne ndani ya miaka mitano na ushindi dhidi ya Atletico Madrid wanaoshika nafasi ya tatu Jumapili utatosha kukipa faraja kikosi cha Tito Vilanova.
 
Barca ina pointi 88 ilizovuna katika mechi 34, na Real ina 80 katika mechi 35 ikiwa nafasi ya pili. Atletico, inayozidiwa pointi nane katika nafasi ya tatu, imejihakikishia kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao kufuatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Celta Vigo mapema Jumatano.
 
What a record! Cristiano Ronaldo scored his 200th goal for Real Madrid in just his 197 appearance
Rekodi gani! Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake la 200 Real Madrid katika mechi 197
 
No 200: His indirect free-kick from inside the Malaga box put Real 2-1 ahead
Bao la 200: Shuti lake la mpira wa adhabu ni bao la 200 Real
Mechi zote zimesogezwa mbele kwa ajili ya fainali ya Kombe la Mfalme kati ya Real na Atletico Mei 17.
 
Beki wa kati, Raul Albiol alitangulia kuifungia Real dakika ya tatu Uwajnja wa Bernabeu kabla ya Roque Santa Cruz, ambaye katika ushindi wa Malaga wa 3-2 nyumbani dhidi ya Real Desemba kusawazisha.
 
Mechi ilibadilika dakika ya 21 wakati beki wa Malaga, Sergio Sanchez alipotolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumuangusha Ronaldo kwenye eneo la hatari.
 
Hata hivyo, mkwaju wa penalti wa Mreno huyo uliokolewa na Willy Caballero, ambaye alijiumiza katika harakati za kuokoa mchomo huo na kumpisha Carlos Kameni, Ronaldo akafunga kwa mpira wa adhabu dakika ya 26.
 
Lilikuwa bao lake la 200 tangu ajiunge na Real kutoka Manchester United mwaka 2009.
 
Mesut Ozil akafunga na kufanya 3-1 kwa Real dakika ya 34, Vitorino Antunes akaipunguzia bao moja Malaga dakika mbili baadaye na baadaye Ronaldo akamtengenezea Karim Benzema kufanya 4-2 karibu na mapumziko.
 
Kipindi cha pili Luka Modric alifunga la tano kwa shuti la mbali dakika ya 63.
 
Beki wa kati wa Malaga, Martin Demichelis akaonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 73 kwa kumchezea rafu Ronaldo na Ozil akatoka nje zikiwa zimebaki dakika 10 baada ya kuumia goti la mguu wa kulia na kuwafanya Real wabaki 10, kwani walikuwa tayari wamekamilisha idadi ya wachezaji wa kubadilisha.
 
Uwanja ulikuwa mtupu tayari wakati Angel Di Maria aliyetokea benchi alipohitimisha karamu ya mabao ya Real dakika za lala salama.
 
Off: Malaga defender Sergio Sanchez is shown a red card after just 21 minutes
Nje: Beki wa Malaga, Sergio Sanchez akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 21
 
Confounded: Players surround the referee after he gave the match-changing decision
Nzugwenzugwe: Wachezaji wakimzonga refa baada ya kujichanganya katika maamuzi yake