Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Monday, 3 June 2013

BABA MZAZI WA MWISHO MWAMPAMBA ARUDISHA KADI YA CHADEMA NA KUCHUKUA YA CCM!!


Baba mzazi mzee Mwampamba akirudisha kadi ya chadema mbele ya Jemedari Mwigulu Nchemba nyumbani mlowo morogoro......

Monday, 20 May 2013

SPIKA WA BUNGE AAMURU KUFUTWA KWA HOTUBA YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE LISITISHWE JANAASUBUHI

 


Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Anne Makinda, ameamuru kambi ya upinzani kuyaondoa maneno yote yaliyomo kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa 14 katika hotuba rasmi ya Kambi ya upinzani iliyosmwa na mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu,’ ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Mh. Makinda ametoa amri hiyo baada ya Kamati ya Kanuni ya Bunge kujadili hotuba hiyo na kubaini kuwa ina kauli za uchochezi; na kusema kuwa kuwa Bunge sio sehemu kugombanisha wananchi, hivyo maneno yote ya uchochezi hayaruhusiwi.
 
Katika hotuba hiyo, Mh. Mbilinyi aliishutumu serikali kuhusika na kuteka nyara waandishi wa habari, kauli iliyopelekea Spika Makinda kuahirisha Bunge.

"IVI WEWE ZITTO KABWE UNADHANI UNASTAHILI KWELI KUWA RAIS ?"....LOVENESS DIVA


Baada  ya  kutangaza  kumpiga  chini  Mh.Zitto Kabwe, Loveness  Diva  ameamua  kumchokonoa  tena  kwa  kumkejeli  kuhusu  uamuzi  wake  wa kugombea Urais.....

Huu  ni ujumbe wake aliouweka instagram: 

 ".Ivi  kwa akili yako unadhani  unastahili  kweli  kuwa Rais mteule wa taifa  hili....??

"Usiponijibu nikaridhika, basi  ntakuchukulia  kama  mtu mwenye upeo finyu asiyejua alitendalo.."

HII NDO KAULI YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE LISITISHWE GHAFLA LEO KUOGOPA UCHOCHEZI

Muda mfupi uliopita spika wa bunge, Anna Makinda amelazimika kusitisha shughuli za bunge mwanzoni tu mwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikisomwa na waziri kivuli wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi aka Sugu.


Kauli kwenye hotuba hiyo iliyobabisha spika wa bunge asitishe shughuli za leo hadi jioni ilisema, 

“Tanzania imegeuka chini ya usimamizi wa wizara ya serikali hii ya CCM kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua.”
SEHEMU YA HOTUBA  HIYO:

MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,

Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye uwezo na malezi bora, linathamini utamaduni wake na linakuwa mahiri katika michezo ifikapo mwaka 2025.” Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni ‘kuendeleza utambulisho wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari, kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.’

Mheshimiwa Spika,

Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Serikali hii ya CCM imeshindwa kutekeleza dira na dhamira iliyotajwa katika maandiko ya kisera ya Wizara. Badala yake, chini ya usimamizi wa Wizara hii, Tanzania imegeuka kuwa taifa lisilotaka watu kuhabarishwa vizuri juu ya matendo ya watawala. 


Tanzania imegeuka kuwa taifa linalofungia magazeti yanayofichua ufisadi, uchafu na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa viongozi, watendaji na watumishi wa Serikali hii ya CCM. Tanzania imegeuka, chini ya usimamizi wa Wizara na Serikali hii ya CCM, kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa kwa kuwang’oa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua. 

Tanzania sio nchi inayoandaa vijana wake tena. Haiwapi tena elimu bora wala kuwapatia maarifa, uwezo na malezi bora; ni nchi isiyowawezesha wala kuwathamini vijana wake; ni nchi inayoruhusu vijana wake kunyonywa na kutoendelezwa; na ni taifa ambalo limeachia utamaduni utambulisho wake kama taifa kupotea kabisa. Aidha, katika fani ya michezo ya aina zote, Tanzania imeporomoka kutoka taifa lililokuwa linaheshimika kimataifa katika miaka ya sabini na kuwa alichokiita rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ‘kichwa cha mwendawazimu’ ambacho kila kinyozi anajifunzia kunyolea!


2. UHURU WA UHARIRI NA USALAMA WA WANAHABARI

Mheshimiwa Spika,

Kwa masikitiko makubwa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inalitaarifu Bunge lako tukufu kwamba sasa Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya fedheha (The List of Shame) ya mataifa ambayo taaluma ya habari ni taaluma ya hatari kwa wale wote wanaoitumia kama sehemu ya wajibu wao kwa taifa na kama ajira yao. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari Ulimwenguni (the Committee to Protect Journalists - CPJ) iliyotolewa mwaka huu 2013, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa CPJ mwaka 1992, Tanzania imeingizwa kwenye orodha ya nchi 20 ambazo ni hatari kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao kutokana na hatari ya kuuwawa kwa mwaka 2012 (20 Deadliest Countries in 2012). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ilishikilia nafasi ya 7 ulimwenguni kati ya nchi 20 zinazoongoza kwa kuhatarisha maisha ya waandishi wa habari.

Mheshimiwa Spika,

Kwa mujibu wa taarifa ya CPJ, tishio kubwa kwa waandishi wa habari duniani ni kuuwawa kwa kutekwa na kuteswa na/au kutishiwa maisha. Aidha, Serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama ni washiriki wakubwa wa mauaji ya waandishi wa habari. 

Kwa mujibu wa takwimu za CPJ, kati ya waandishi waliouwawa mwaka 2012, karibu ya 20% waliuwawa ama na maafisa wa serikali au na majeshi yake. Karibu idadi hiyo hiyo ya waandishi wa habari waliuawa kwa sababu ya kufuatilia taarifa za kiuchunguzi na za hatari. Taarifa hiyo inaonyesha kwamba hadi kufikia Aprili 2013, waandishi wa habari wapatao 30 tayari wamekwishauawa ulimwenguni wakati wakitimiza wajibu wao; wakati mwaka 2012 waandishi wa habari 103 waliuwawa ulimwenguni kote.

Mheshimiwa Spika,
Taarifa ya CPJ inaungwa mkono na ushahidi wa matukio mengi yanayodhihirisha kwamba maisha ya waandishi wa habari wa Tanzania yako hatarini kutokana na vitendo na vitisho kutoka kwa Serikali na watendaji wake ambao hawataki kusikia ukweli dhidi yao ukianikwa hadharani. Kudhihirisha kauli hii tunaomba kumnukuu mwanahabari mahiri na mmoja wa wahanga wa vita dhidi ya wanahabari na uhuru wa habari hapa nchini, Mzee Ndimara Tegambwage:

“Mwaka 2006, waliojiita wananchi wakazi wa jiji la Mwanza, walikusanywa na wenye uwezo kufanya maandamano makubwa kwa walichoita ‘kupinga mwandishi Richard Mgamba kuandika uongo’ na kudai kwamba alikuwa Mkenya na ‘siyo raia wa Tanzania.’ Desemba 2009, mwandishi Frederick Katulanda wa Mwanza, alivamiwa nyumbani. Wavamizi walikuwa wakipaza sauti na kudai kuwa ana nyaraka za akaunti za benki za Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Walikuwa na mapanga. Walikuwa wakichagizana kwa kusema, “Kata kichwa! Kata kichwa!” Waliondoka na mafaili. Walimwachia kilema mguuni na makovu mikononi.

“Mwezi Septemba, 2010 wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, katika eneo la Nyambiti, Jimbo la Sumve wilayani Kwimba, mkoani Mwanza, mwandishi Frederick Katulanda alivamiwa na kupigwa na watu wapatao 15 waliojiita “Green Guard” - wa “chama cha kijani.” Katika “kumshughulikia,” Katulanda anasema, walikuwa wakionyesha kuwa na ujuzi mkubwa wa judo na karate huku wakidai kuwa anawaandika ‘vibaya’ Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Mwaka 2011 mwandishi Richard Massatu alikutwa amekufa katika eneo la Igoma, jijini Mwanza. Vyombo vya habari viliripoti kuwa macho yake yalikuwa yametobolewa na kuwekwa gundi aina ya super glue; mguu wa kushoto na mbavu vilikuwa vimevunjika. Vyombo vya habari viliripoti kuwa Massatu aliyekuwa mmiliki na mhariri mkuu wa gazeti la Kasi Mpya (sauti ya umma), alionekana mara ya mwisho usiku wa kifo chake akiwa na maofisa wa polisi na usalama katika baa iitwayo Cross Park katika eneo la Igoma.

“Tarehe 3 Januari, maiti ya mwandishi Issa Ngumba iliokotwa katika pori la mlima Kajuruheta, kijiji cha Mhange, wilayani Kakonko katika mkoa wa Kigoma.Ngumba alikuwa mwandishi wa habari wa Redio Kwizela. Tangu mwezi uliopita Machi, mwandishi wa habari Erick Kabendera anayeishi Dar es Salaam, anaishi kwa wasiwasi. Wazazi wake waishio Bukoba, wamehojiwa na ‘ofisa usalama’ kwa kile kilichoitwa ‘uhalali wa uraia wao.’

“Kuuwawa kwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Luninga cha ITV, John Lubungo ambaye alikuwa mfuatiliaji mahiri wa habari zinazohusu wafanyabiashara au biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo inadaiwa kufanywa na watu wakubwa nchini, wakiwemo vigogo serikalini. 

Kuna orodha ndefu ya waandishi wa habari waliotishwa na wanaoendelea kutishwa; waliopigwa na polisi na askari magereza (Ukonga, Dar es Salaama) kwa tuhuma mbalimbali; waliotishiwa maisha kwa simu na hata kwa kufuatiliwa na watu wasiowafahamu.”

Kwa sababu ya uadilifu na kutopenda kujikweza, Mzee Tegambwage hakutaja shambulio la tindikali na mapanga dhidi yake na mwandishi mwenzake Saed Kubenea wa gazeti la Mwanahalisi, ambalo baadae lilifungiwa na Serikali hii ya CCM.

Mheshimiwa Spika,

Katika Maoni yake wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ya tarehe 3 Mei mwaka huu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilielezea kwa kirefu jinsi ambavyo Serikali hii ya CCM imekuwa tishio kwa maisha ya waandishi wa habari na kwa uhuru wa habari katika nchi yetu. 

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilirejeaRipoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi Iliyoteuliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Kuchunguza Mazingira Yaliyopelekea Kuuawa kwa Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi Septemba 2, 2012 Katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa, iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), taasisi mbili huru zinazojihusisha na masuala ya habari Tanzania.

Kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF, matokeo ya uchunguzi wao “... yanadhihirisha bila wasi wasi kwamba polisi kwa makusudi waliwavurumisha waandishi waliotoka Iringa wakati wakikusanya habari za shughuli za CHADEMA katika kijiji cha Nyololo.

 Zaidi ya hapo, Daudi Mwangosi mwenyewe aliuawa akiwa mikononi mwa polisi huku wakisimamiwa moja kwa moja na Kamanda (wa Polisi wa Mkoa wa Iringa SACP Michael) Kamuhanda.” Ripoti hiyo inaelezea jinsi Marehemu Mwangosi alivyouawa: “Alipoangalia nyuma, Daudi Mwangosi aliona kikundi cha polisi wakimpiga mwandishi mkuu wa gazeti la Nipashe wa Iringa, Godfrey Mushi.... Wakati mwandishi Godfrey Mushi akiwa bado anapigwa na polisi, marehemu Mwangosi aliwakimbilia akiwaomba waache kumdhuru zaidi Mushi kwa kuwa alikuwa mwandishi tu. 

Polisi hawakumsikiliza. Badala yake wakamburuta mwandishi huyo ambaye tayari alikuwa amepoteza fahamu na kumweka kwenye gari lao na wakamgeukia Daudi Mwangosi mwenyewe, wakampiga kwa nguvu mpaka akapoteza fahamu.”

Hata amri ya Mkuu wa Kituo cha Polisi Mafinga Mwampamba kuwataka askari polisi waache kumpiga marehemu Mwangosi haikusikilizwa na askari hao. Ili kujiokoa, marehemu Mwangosi alimkumbatia OCS Mwampamba na “baadaye kumwangukia miguuni mwake kuepuka kipigo zaidi.” 

Kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF, “picha za mgando zinaonyesha polisi mmoja akipiga bomu la machozi tumboni mwa marehemu Mwangosi kwa karibu kabisa.” Bomu hilo liliusambaratisha mwili wa marehemu Mwangosi aliyekufa papo hapo. Kwa sababu marehemu Mwangosi alikuwa chini ya miguu ya OCS Mwampamba, “naye pia alijeruhiwa vibaya.”

Mheshimiwa Spika,

Sio MCT/TEF pekee zilizofanya uchunguzi wa mauaji ya Marehemu Mwangosi. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nayo ilitoa Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya Uchunguzi wa Tukio Lililopelekea Kifo cha Daudi Mwangosi Kilichotokea Septemba 2, 2012 Kijijini Nyololo, iliyobaini kwamba Marehemu Mwangosi “... alizingirwa na askari, aliteswa na hatimaye ... alipigwa bomu na kufa papo hapo.” Aidha, kwa mujibu wa Taarifa hiyo, “... 


Tume imejiridhisha kuwa tukio la lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi limegubikwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.” Taarifa ya Tume inafafanua kuwa, “... 


Tume imejiridhisha kuwa Jeshi la Polisi limevunja haki ... ya kuishi, haki ya kutoteswa na kupigwa, haki ya usawa mbele ya sheria na haki ya kukusanyika na kutoa maoni.”

Mheshimiwa Spika,

Inaendelea..
 
Spika amesitisha bunge hilo ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo kuondoa kauli za uchochezi.

AUDIO:Bofya PLAY

"MNAOTAKA URAIS ANZENI KUPITAKUPITA ILI MTAMBULIKE".....HII NI KAULI YA RAIS KIKWETE


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amefungua milango kwa kuwataka baadhi ya watu ndani ya chama hicho wanaowania urais mwaka 2015 kuendelea na mchakato huo.

Rais Kikwete amewatahadharisha watu hao kuendesha kampeni zao kwa ustaarabu pasipo kuibua chuki wala kujenga makundi ambayo alisema ni hatari kwa kuwa yanaweza kukipasua chama. Rais Kikwete aliyasema hayo katika mkutano ndani wa wabunge wa chama hicho uliofanyika jana katika ukumbi wa CCM (white house) mkoani Dodoma.

Mkutano huo ambao ulianza saa 3.00 asubuhi ulilenga kujadili masuala mbalimbali ya taifa ikiwamo utekelezaki wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho katika majimbo na ahadi mbalimbali za viongozi wa taifa.
 
Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya ukumbi huo kilieleza kuwa Rais Kikwete aliwataka wanachama wenye nia ya kugombea urais kuwa na tahadhari na watu aliowaita vishoka wa siasa.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, Rais Kikwete alisema watu wa aina hiyo wana tabia ya kula huku na huku kwa kujiingiza katika kambi zaidi ya moja.

“Tuangalie makundi ya urais 2015 yasishambuliane kwa kuvunja chama, wenye nia hiyo ya kugombea waendelee na mikakati yao bila kujenga chuki kwa makundi mengine.

“Katika hatua hiyo, pia mkumbuke kuwa katika kambi hizo za urais zinatakiwa kujitizama wao na wafuasi wao maana wafuasi wengine hawaaminiki, ” alisema Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, miongoni mwa ajenda alizokuwa nazo Rais Kikwete ni pamoja na suala la urais na utendaji wa wabunge majimboni.

Rais Kikwete aliwataka wabunge wa chama hicho kubadili mwenendo wa kuyatelekeza majimbo yao na badala yake akawahimiza kujenga tabia ya kutembelea majimbo yao mara kwa mara.

“Hili JK amelisemea kwa ukali kwamba tabia ya baadhi ya wabunge kuhamia mijini na kutelekeza majimbo yao ni hatari kwani mwisho wa siku wananchi watawanyima kura na kuzipeleka upinzani.
 
Pia alikemea tabia ya baadhi ya wabunge kununa na kuwachukia watu wengine wenye nia ya kugombea katika majimbo yao. Akasema mbunge asiyetimiza wajibu wake kwa wananchi wake na bungeni ni vigumu kubaki.

“Wanatakiwa kurudi majimboni kwao kusimamia ilani ya chama pamoja na ahadi zao walizoahidi na zile za viongozi wa chama na Serikali ikiwamo ahadi zake kama rais,” alisema.

Kuhusu suala la ukosoaji, Rais Kikwete alisema wabunge wa chama hicho wana wajibu wa kuikosoa Serikali yao lakini akaonya aina ya ukosoaji wenye lengo la kuibomoa Serikali.

“Mnatakiwa kuisimamia Serikali na kuikosoa bila kuibomoa, lakini kuna baadhi yenu mmekuwa mkiibomoa Serikali kwa jinsi mnavyochangia huko bungeni… hilo si jambo jema hata kidogo, waachieni wale wenzetu,”alisema Kikwete.

Chanzo hicho kilieleza kuwa wabunge wamekuwa hawaridhishwi na utendaji wa baadhi ya mawaziri ambao walisema ni mizigo na kutaka waondolewe katika nafasi zao.

Chanzo hicho kilitaja majina ya mawaziri hao wanaodaiwa kuwa ni mizigo kuwa ni Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. David David Mathayo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenera Mkangara.

Baadhi ya wabunge walimtaka Rais Kikwete kudhibiti ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri mbalimbali nchini, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa.

“Rais anatakiwa kukunjua makucha yake kuondokana na uozo huu katika halmashauri zetu. Haiwezekani waendelee kunyamaziwa, tunatakiwa kuimarisha chama kwa kuangalia namna Serikali inavyoweza kutimiza ahadi kwa wananchi,” kilisema.

Kiliendelea kusema. “Serikali iweze kusaidia katika kutimiza ahadi kwa kutelekeza ilani ya chama, viongozi wa vijiji, kata na vitongoji kuanza kulipwa mshahara maana wamejitolea kwa muda mrefu hivyo huwalazimu kupata ushawishi kutokana na njaa,” kilisema.

Imeelezwa kuwa katika kikao hicho kinachoendelea kitakuwa na ajenda nyingi ambazo zitaibuliwa na wabunge.

Hizo ni pamoja na maslahi ya wabunge, utendaji kwa baadi ya mawaziri na aina ya ukosoaji inayofanywa na baadhi ya wabunge wa chama hicho.

Baada ya mapumziko ya mchana, kikao hicho kiliendelea kwa wabunge kupata nafasi ya kujadili hoja mbalimbali kutokana na hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa asubuhi.

Rais Kikwete anakutana na wabunge hao wakati wenyewe wanaonekana kugawanyika kutokana na kuwapo kundi la wabunge wanaoitetea Serikali na wengine wanaoikosoa.

Miongoni mwa wabunge wanaoikosoa Serikali ya chama hicho waziwazi ni Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy.

Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa wabunge hao machachari walichanwa hadharani na baadhi ya wabunge wanaoiunga mkono Serikali hali inayoonyesha kuwa wabunge hao si wamoja.

Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba alisimama na kueleza kuwa anashangazwa na aina ya ukosoaji unaofanywa na wabunge hao na kusema. “Kama hawataki kufuata maelekezo ya chama wahame,” alisema.

Sunday, 19 May 2013

ZITTO KABWE ALIVYOFUNIKA JANA TABORA , UMATI MKUBWA WAJITOKEA KUMWONA. CHEKI PICHA HAPA

Embedded image permalinkEmbedded image permalink
Embedded image permalinkEmbedded image permalink

MWENYEKITI WA CCM, RAIS KIKWETE AFANYA KIKAO MUHIMU NA WABUNGE WA CCM LEO MJINI DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini wakati wa kikao chake na wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine kushoto ni Spika wa Bunge Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kikao chake na wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine kushoto ni Spika wa Bunge Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula.

  Wabunge wa CCM wakiwa kwenye kikao chao na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete leo kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

 Wajumbe kwenye kikao hicho wakibadilishana mawazo ukumbini. Walioketi mbele, Kushoto ni Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakiah Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migoiro na Mbunge wa Urambo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai na Katibu wa NEC Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib kwenye kikao hicho.

 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro(kulia) akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Mbunge wa Same Anne Kilango Malecela.

 Mbunge wa Songea na Waziri wa Mambo ya Ndani,Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akitaniana kuhusu Uyanga na Simba na Mwenyekiti wa Simba, Mbunge wa Tabora Aden Rage nje ya ukumbi kabla ya kuanza mkutano huo. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya.










PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA WAFUNIKA BOVU CHEKI HAPA TASWIRA NZIMA ILIVOKUWA

Picha juu ni Maelfu ya wananchama wa Chadema Wakiwa kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Arusha Jana kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani wa kata nne; Elerai, Kaloleni, Themi na Kimandolu ambazo madiwani wake walifukuzwa uanachama na chama hicho huku kikitamba kuwa hakina uchaguzi Arusha ila CCM ndio wenye uchaguzi.

Saturday, 18 May 2013

ANGALIA PICHA ZA UZINDUZI WA KAMPENI YA UDIWANI ARUSHA



"MIMI SIYO MSAGAJI....NIPO TAYARI KUWATAJA WANAUME NILIOLALA NAO"...HALIMA MDEE


Kupitia season mpya ya Clouds Fm, ndani ya so so fresh na fetty, Mh Halima Mdee jana amefunguka juu ya swali aliloulizwa kuhusu story zilizosambaa kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja.

Hii  ndo  kauli  yake:
"Unajua huwezi kuzuia watu kusema, na mimi huwa sihangaiki na watu wanasema nini, lakini ukitaka kumjua Halima unaweza ukamchunguza kirahisi sana, kwa kumuangalia alipotoka, historia yake na mahusiano yake, ambayo mengine ni wazi sana watu walikuwa wanayajua...
 
"Watu wanapenda ku speculate pale ambapo wanaona kitu ambacho hawataki  kuona, sasa hilo swala lilishaandikwa sana, nadhani walioandika baadae wakaja kuomba radhi kwasababu waligundua wameandika kitu kisicho sahihi, probably kutokana na sauti yangu you know, probably kutokana na tembea yangu, kwasababu mimi nimekulia kwenye familia ya wanaume watupu umeona eeh,...

"Mimi nimekuwa ni mpambanaji tokea utotoni, kwasababu nimezungukwa na jeshi la kibabe, thats who iam, lakini mtu anaetaka kumjua Halima na ana uhuru tu, hata akitaka niwatajie list ya watu wangu i can do that....

"Lakini sidhani kama is their damn business, cause ma life is personal, na wakitaka kuchunguza wachunguze kwa mpango wao na watapata taarifa, kwa uhuru tu, na wanaweza wakatoa tangazo kwamba jamani watu waliowahi kuwa na uhusiano na huyu if any wajitokeze....

"Watajitokeza kama wapo upande huo, watajitokeza kwasababu sasa hivi si dunia huru bana."

Zitto: Tafuta Mbunge wako, Mwambie Asikubali Maamuzi haya ya Serikali - Gesi Sio Viazi, Haiozi

Leo wabunge tumealikwa kwenye semina kuhusu sera ya Gesi Asilia. Tumegawiwa tayari nakala zetu, tena zipo kwenye lugha ya kimombo. Ikumbukwe kwamba kuanzia tarehe 22 - 23 Mei 2013 kutakuwa na mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Semina hii ni maandalizi ya Bajeti hii.

Jambo la kushangaza ni kwamba wakati sera ya Gesi Asilia ipo kwenye rasimu na ndio kwanza wabunge tumeletewa kutoa maoni, Serikali tayari imetangaza tena kugawa vitalu vya Mafuta na Gesi kwenye Bahari kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini.

Zabuni hii mpya ya vitalu vya utafutaji imetolewa wakati kuna maamuzi ya Bunge kuzuia ugawaji huu mpya mpaka sera ya Gesi Asilia na Sheria ya Gesi vikamilike. Haraka hii ya serikali kugawa vitalu bila sera wala Sheria inatoka wapi? Nitashangaa sana wabunge kukimbilia posho za semina hii na kuhalalisha maamuzi yasiyo zingatia maslahi ya Taifa Kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Uamuzi wa kugawa vitalu vipya bila kwanza kuwepo Kwa sera na Sheria mpya unapaswa kupingwa Kwa Nguvu zote.

Tafuta mbunge wako, mwambie asikubali maamuzi haya ya serikali.

Tumalize kwanza sera na Sheria ndio tugawe vitalu vipya. Gesi sio viazi, haiozi.

Friday, 17 May 2013

DR. MWAKYEMBE NA COME ON FU@@Y YOU (SERUKAMBA) WAVAANA

Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe 


Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameingia katika msuguano wa chinichini na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba ambaye alidaiwa kuongeza maneno kwenye hotuba ya kamati yake yaliyokuwa yakimlenga waziri huyo binafsi.
 
Kutokana na hali hiyo, hotuba iliyokuwa isomwe na Serukamba kama maoni ya kamati baada ya Dk Mwakyembe kuwasilisha hotuba yake, ilibadilishwa dakika za mwisho na kusainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Juma Kapuya.
 
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo (ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe) alisema waliamua kuunda kamati ndogo ya wabunge wanne kusahihisha lugha iliyotumika katika kuandaa maoni ya kamati hiyo kuhusu Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.
 
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wajumbe waligundua kuwa lugha iliyotumika ililenga kushambulia moja kwa moja Dk Mwakyembe ndani ya Bunge jambo ambalo lilkuwa kinyume cha makubaliano ya kamati.
 
Hata hivyo, Serukamba akizungumza na gazeti hili alikana kubadili hotuba hiyo na kuongeza kuwa; “Mimi nimerudi jana, kwa kawaida kamati ikishajadili suala la hotuba kuandikwa tunamwachia Katibu na akimaliza anairudisha kwetu wabunge. Hivyo nilichokisoma ndicho tulichokubalina na wajumbe wa kamati hiyo.”
 
Aliongeza: “Msitake kunigombanisha na mheshimiwa Waziri, mimi ndiyo kwanza nimeingia asubuhi hii hakuna kilichobadilika katika hotuba hiyo.”
 
Gazeti hili lilifanikiwa kuona nakala mbili za hotuba za kamati, moja ikiwa na saini ya Serukamba na nyingine ikiwa imesainiwa na Profesa Kapuya na zote zina tarehe inayofanana ambayo ni Mei 16, 2013.
 
Kwa upande wake Kapuya katika majibu ya maandishi kwa gazeti hili alisema si kweli kwamba ziliandikwa hotuba mbili. “Habari hizo hazina ukweli, kamati yangu ina utaratibu wa kuandaa hotuba yetu na ikishakamilika tunateua kamati ndogo ambayo inapitia hotuba hiyo kabla ya kuisoma,”alisisitiza Profesa Kapuya.
 
Majibu ya Serukamba na Kapuya yanatofautiana na kauli ya Dk Mwakyembe ambaye aliliambia gazeti hili kwamba pia alipata taarifa za kuwapo kwa mpango huo kutoka kwa “watu wanaojua na kuthamini kazi yake.”
 
“Siyo kila mtu anaweza kukuchukia huwezi kunyimwa maneno, watu wenye imani na mimi walikuja kunipa taarifa na wakanipatia ile aliyokuwa ameandika yeye…. ana bahati sana nilikuwa namsubiri kwa hamu aisome hiyo hotuba yake nilipanga kumchanachana pale pale asingeamini,”alisisitiza Dk Mwakyembe.
 
Alipoulizwa kwa nini anafikiri mwenyekiti huyo ameamua kumfanyia hivyo, Dk Mwakyembe alisema; “Siwezi kujua lakini naamini hizi ni mbio tu za mwaka 2015.”
 
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema hafahamu kuhusu suala hilo. “Ninachofahamu ni kwamba Serukamba alikuwa amesafiri kwenda China na mimi nilimwona siku hiyo akisoma maoni ya kamati yake, kama kulikuwa na tatizo hilo pengine litakuja baadaye ofisini kwetu,”alisema Ndugai kwa simu.
 
Ilikuwaje?
Habari zinasema licha ya kwamba Serukamba alikuwa nje ya nchi, alihusika katika kuandaa rasimu ya awali ya taarifa ya kamati ambayo yeye alisaini.
 
Hata hivyo wakati akiwa bado hajarejea nchini, wajumbe wa kamati yake walibaini kwamba katika hotuba hiyo kulikuwa na lugha ya kumuhoji zaidi waziri pamoja na Serikali badala ya kushauri, huku baadhi ya kauli zikionyesha kumlenga Dk Mwakyembe binafsi.
 
Wajumbe hao walilalamika kwamba maneno hayo yaliyokuwa yakimshambulia waziri ni kinyume na walivyokubaliana hivyo waliamua kuunda kamati ya watu watatu ambao ni wajumbe wa kamati hiyo ili kufanya marekebisho.
 
“Hatua ya kuunda kamati hiyo ndogo ilifikiwa Jumatatu wiki hii, maana tulibaini kwamba lugha iliyotumiwa haikuwa sahihi, sisi kazi yetu ni kuishauri Serikali na si kuhoji maswali, maswali unaweza kuhoji wakati wa kuchangia mbunge mwenyewe lakini si kwa kuandika katika maoni ya kamati, “kilieleza chanzo hicho.
 
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge toleo la 2007 ya 114(18), Kamati ya Kudumu ya Bunge inaweza kuunda kamati ndogo kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli zake, kadri itakavyoona inafaa na kila kamati ndogo itapangiwa kazi zake na kamati ya kudumu husika.
 
Wajumbe hao ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ramo Makani na Wabunge wa Viti Maalumu, Rita Kabati na Zarina Madabida wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hotuba hiyo baada ya kukamilika ilisainiwa na Profesa Kapuya na hiyo ndiyo iliyosomwa bungeni.


MWANANCHI

WANAWAKE JIJINI MBEYA WAMVAA MCHUMBA WA DR. SLAA BAADA YA KUMKASHIFU MKE WA RAIS KIKWETE


UMOJA wa wanawake  wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya(UWT) umemshukia Bi.Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.


Hatua hiyo inatokana  na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri   Rais ambaye ni mume wake  kuiongoza nchi vizuri .

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Bi.Priscilla Mbwaga wakati  akitoa Tamko   kwa waandishi wa habari juu ya Matusi ya wazi yaliyotolewa na Bi.Mushumbusi   kwa Mke wa Rais katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Wilayani Mbozi Kata ya Vwawa Mkoani hapa.

Bi.Mbwaga alisema kuwa katika mikutano yake ya Hadhara Bi.Mushumbusi alidai kuwa  mama Salma Kikwete  ameshindwa kumshauri  mume wake kuingoza nchi na kuacha Twiga wakiwa wanakunjwa na kuondoka na kwamba yeye akiwa Ikulu hataacha kumshauri mume wake Dkt.Slaa katika masuala ya kuingoza Nchi

 
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kama umoja huo wanalaani  vikali lugha chafu na za kichochezi zinazopandikizwa  chuki miongoni mwa jamii ya watanzania .

Alisema kuwa kama umoja wa wanawake  wanalaani matusi hayo na kwamba umoja huo  ulifuatilia  mikutano  hiyo na kugundua kuwa ilikuwa imetawaliwa  na  matusi badala ya kutoa sera  kwa wananchi kuwa wanataka kufanya nini.

“Sisi kama umoja wa wanawake  Mkoa tunaeleza umma  ambao una imani na  kuwa katika utamaduni   na maadili  yao hawapendi  na wala hawajazoea kusikia matusi  katika  jamii yao hivyo wakiangalie vizuri na kwa  makini Chadema  kuwa  cha hicho kina  watu  wa maadili gani , mahali  pote  siku zote  na miaka  yote  ni matusi,kuongea uongo, uzushi  na kashfa wasimamapo majukwaani “alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha Bi.Mbwaga alisema kuwa wanawake wa mkoa wa Mbeya  wanadhani kuwa kauli ambazo zimetolewa na  Mushumbusi ni  ni za kuwadhalilisha wanawake wote wa Tanzania  kwani Mama Salma ni Kiongozi wa juu pamoja
na Mushumbusi .


“Tunamshangaa sana  Mushumnbusi anaposimama majukwaani na kutoa kashfa nzito za namna hii ni  kama nani kwa wanawake  wa Tanzania 'alihoji Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani hapa (CCM),Bw.Amani Kajuna  alisema  kauli aliyotoa Dkt.slaa kuwa Rais Kikwete  ana Udini ni ulaghai  mkubwa  ambao anaufanya kwa wananchi  na kuendelea kuiweka nchi katika mazingira magumu .

“Kama vijana  tunatambua kuwa  Rais Kikwete ni kiongozi wa watanzania, na kwamba hana sifa ya Udini hii ajenda inaanzishwa kisiasa ili kujipatia umaarufu wa bure wa kudhani kuwa ndiyo njia ya kuwapeleka ikulu  mwaka 2015 jambo ambalo halitawezekana ,maana  watanzania hawataweza kukubali"
alisema Mwenyekiti huyo.


Hata hivyo Bw.Kajuna aliendelea kusema kuwa Dkt. Slaa amekuwa akimtuhumu  Rais Kikwete kuwa  ni FREEMASON , “hebu tumuulize huyu mtu amekutana lini na Rais kwenye iman hiyo” na kwamba katika uongozi wake watanzania  wameona miradi mikubwa  ya maendeleo ya nchi yetu kwa ukuaji wa wa pato la Taifa.

CHADEMA ISITEGEMEE KUSIFIWA NA CCM HATA SIKU MOJA


Kiuhalisia chadema imekuwa msitari wa mbele katika kuuamsha umma juu ya matukio ya uhujumu uchumi unaotokea katika nchi hii kwa muda sasa na kufanya wananchi kuelewa kwa nini nchi hii ni maskini na viwanda vyote vimefishwa badala ya kuendelea na kujenga vingine vipya. Chadema ilichofanya si haba kwani hali ilivyo sasa hata katika vijiji ni hamasa tupu ya mabadiliko japo kuna watu wameketi huko waliko na kujifanya hawaoni hilo, huku katika vijiji vyetu vilivyo remote kabisa mambo yamegeuka kwa mfano katika vijiji vya huku geita ambako kutoka kijiji kimoja hadi kingine ni pori kubwa mambo si haba.

naomba nirudi kwenye topic: Kwa misingi hiyo niliyoeleza hapo juu ccm wanafanya kila lililo ndani ya uwezo wao ili kupotosha umma kuwa chadema ni chama cha fujo, kikanda, kikabila, udini na uhanaharakati. Kwa hali hiyo mimi binafsi napenda kuwashauri viongozi wa chadema kutokubali kucheza muziki wa ccm kwani muziki huo unahitaji mtu uwe umechanganyikiwa ndo uweze kwenda na hiyo beat. Kwetu sisi tuliokuwa kwenye ground tunajua hali halisi iliyoko huku.

Kwa kuanzia napenda kuwaasa viongozi wa chadema wamsome na kumuelewa nape ambaye alisifia mchakato wa katiba, ikumbukwe kuwa mambo yote yaliyo mabaya ccm huwa wanayasifia kwa kuwa ni wao waliyoyatengeneza kwa kulinda masilahi yao binafsi. Kwa hivyo chadema wanatakiwa suala hili walivalie njuga ili kutowapa muda wa kupumua kwani hata wananchi wenyewe wanaelewa ni nini kilichofanyika. Sisi tulioko huku vijijini tunaendelza kazi kama kawaida ya kumwaga sumu kwa wananchi, na tumefanya mkakati wa kuelimisha vijana wa sekondari kuelewa haya mambo kiundani zaidi.

Nisiwachoshe wasomaji na wachangiaji nitarudi tena kuendelea na nilichokimaanisha zaidi,
karibuni nyote..
Source:Mdau Jamii Forum

WABUNGE SIMBA WAPANGA MIPANGO YA KUIANGAMIZA YANGA JUMAMOSI HII

Wabunge mashabiki wa klabu ya Simba wanaoshiriki vikao vya Bunge vinavyoendelea jijini Dodoma, jana walifanya kikao Msalato, nje kidogo ya mji lengo likiwa ni kupanga mikakati ya kuhakikisha timu inapata ushindi kwenye mechi ya kufunga msimu dhidi ya Yanga Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa. 

 
Timu hizo zinakutana kufunga msimu, huku Yanga ikiwa tayari imeshatawazwa ubingwa kabla hata ya mechi kumalizika na Simba ikijihakikishia nafasi ya tatu kutegemea matokeo ya mchezo huo.
 
Juzi jioni Naibu Spika Job Ndugai, alitangaza bungeni wakati akisoma ujumbe wa maandishi wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani, aliouandika akitaka Ndugai kuwatangazia wabunge wanaoishabikia timu hiyo kukutana.
 
“Kuna mambo muhimu sana lazima niyatangaze sasa hivi, Mheshimiwa Ngonyani anawatangazia wabunge wote mashabiki wa Simba kesho (jana) wakutane kule wanakokutana Msalato kwa ajili ya kupanga mikakati,” alisema Ndugai.
 
“Hapa nimekaa na mwenyekiti wa Simba, Aden Rage na yeye kaniambia wale wote (Waziri wa Ujenzi John Magufuli) na Naibu wake (Gerson Lwenge) ni Simba pia,” alisema Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba (CCM) wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi.
 
Juzi, Mbunge wa Urambo Magharibi, Juma Kapuya, alimshauri Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage kuwataka yosso wa Simba kuwafunga ‘babu’ zao wa Yanga.
 
Wabunge mashabiki wa Simba ni Rage (Mwenyekiti wa Simba), Ndugai (Kongwa), Ngonyani, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (Urambo Mashariki), Kapuya, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).
 
Idd Azzan (Kinondoni), Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Amos Makala (Mvomero), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge, ( Njombe Magharibi), Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, (Mkuranga) na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli.
 
Wakati huohuo, mashabiki wa Simba wametakiwa wasiwe na hofu na wajazane uwanjani kuona timu yao ikiwaadhiri watani wao wa jadi, Yanga.
 
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ walitamba jana mjini Zanziba kuwa Simba iko imara na itaibwaga Yanga.    

Thursday, 16 May 2013

MSIGWA AGOMA KUMUOMBA RADHI KINANA NA BADALA YAKE AMEMSHAURI AENDE MAHAKAMANI KAMA ANADHANI ALIONEWA

Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amemtaka  katibu mkuu  wa chama  cha mapinduzi (CCM) Bw  Kinana  kutosubiri muda  wa  siku  21 alizozitoa  kumfikisha mahakamani na kudai kuwa  yupo tayari  kwenda mahakamani hata kesho.

Mbunge Msigwa amesema kuwa katika  ukweli  hatakuwa   tayari kumwogopa mtu na kuwa siku  zote atasimama katika  ukweli katika  kupigania maslahi ya Taifa  hili.

Mbunge  Msigwa amesema  kuwa hatua ya katibu mkuu  wa CCM kukimbilia katika  vyombo  vya habari  kutishia  kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika  kupelekewa taarifa  ni  sawa na kumwogopa na  hivyo suala la Kinana kwenda Mahakamani  si  sawa ni  kumtishia nyau mtu mzima.

Msigwa  alisema  Chadema  ina  mawakili  waliojitosheleza na  kuwa hawatanyamaza kusema  ukweli kwa  kuogopa vitisho vyovyote .
 
 Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi  wa  jimbo hilo leo  jioni katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya mikoani
 



 Umati mkubwa  wa  wananchi  wakimsikiliza mbunge  wao wa  jimbo la Iringa mjini
 
 Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji ,Msigwa akiwahutubia  wananchi  wa  jimbo la Iringa mjini

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO ANGALIA TASWIRA ILIVOKUWA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma, May 16, 2013.
 
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Harison Mwakyembe akisoma Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo, Bungeni Mjini Dodoma, May 16, 2013

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu Mjini Dodoma , May 16,2013.
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Joyce Mends-Cole, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mjini Dodoma May 16, 2013.
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata Maelezo kuhusu mizinga ya nyuki iliyofinyangwa kwa udongo kutoka kea Mkurugenzi wa Shirikala African SoilHives Technology la mafinga Iringa, Donald Kalinga (kushoto) kwenye makazi yake Mjini Dodoma May 14,2013. Wengine pichani kutoka kushoto ni Farida Mgalama, Tekla Pila na Beather Mkono, wote ni wananchama wa Shirika hilo
 
Watalaamu wa nyuki kutoka Kampuni ya National Beekeeping Supplies Limited ya Dodoma, David Kamala (kushoto) na Abubakar Salum wakilina asali kwenye shamba la ufugaji nyuki na kilimo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda lililopo Zuzu Mjini Dodoma, May 15, 2013 usiku. Mzinga mmoja ulitoa wastani wa lita 10 za asali.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu