Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Tuesday, 18 June 2013

SABABU ZA JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU YA MABOMU JIJINI ARUSHA MUDA HUU


Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.


Kamanda Sabas amedai  kuwa  jeshi la polisi  liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo wamekaidi agizo hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyoleta  mvutano kati ya viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao baada ya kukaidi amri ya jeshi hilo mabomu yalirindima uwanjani hapo.

Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje...

Jacob Steven (JB) achaguliwa kuwa balozi na Oxfam; Ni katika kampeni yao ya Grow

Mwigizaji anayekubalika zaidi nchini na aliyeshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume 2012/2013 kupitia tuzo za steps entertainment zilizofanyika siku ya tarehe 15/06/2013 jijini Dar es Salaam, Jacob Steven maarufu Zaidi kama JB ama “Bonge la bwana” amechaguliwa kuwa balozi wa shiriki lisilo la kiserikali la Oxfam International linalojihushisha na mambo mbalimbali ya kuondoa umasikini duniani kupitia kampeni yake ya grow kwa upande wa Tanzania.

Usimikaji huo ulioambata na utoaji wa tuzo maalumu kwa watu washindi hao sita wakiwemo Dina Marious wa clouds FM, Mheshimiwa Halima Mdee (Mbunge wa kawe), Mheshimiwa Shy-Rose Bhanji (Mbunge), Mchoraji katuni maarufu Masoud Ally wa Kipanya, Mbunifu wa mitindo Tanzania Khadija Mwanamboka na Blogger maarufu nchini Shamimu Mwasha.

GROW ni kampeni ya kimataifa inayoendeshwa na shirika la Oxfam. Kampeni hii inataka tuoteshe na kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa chakula, uimarishaji wa haki na mustakabali wa wanawake wazalishaji wa chakula na pia kulinda mandhari ya uoto na uhalisia wa sayari yetu.

Dunia inazalisha chakula cha kutosha lakini watu wapatao milioni moja wanalala bila kula kila siku. Mbaya zaidi, idadi kubwa ya hao ni wanawake wazalishaji na watoto.

FREEMAN MBOWE AWAFARIJI WAFIWA, ATEMBELEA ENEO LA MLIPUKO NA KUJULIA HALI MAJERUHI WA SHAMBULIO LA BOMU

Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu (Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Freeman Mbowe na Godbless Lema wakiwa katika Uwanja wa Soweto jana mchana wakati zoezi la kuchukua vipimo mbalimbali likiendelea chini ya usimamizi wa wataalamu toka jeshini.
Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako kwa kitu ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo tanki hilo lilishambuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari hii ya matangazo lina majeraha mawili mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu chenye ncha ambacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.
Dereva wa mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bwana Benny akiwa hospitali.
James Ole Millya na Mbunge Lema wakimjulia hali mmoja wa majeruhi walilazwa hospitali ya Seliani.

SHUGHULI MBALI MBALI ZIKIENDELEA KWENYE FUKWE ZA ZIWA NYASA WILAYANI LUDEWA MKOANI NJOMBE





Shughuli mbalimbali zikiendelea kwenye ufukwe wa ziwa Nyasa katika mwambao wa ziwa hilo kwenye kijiji cha Lupingu, wilayani Ludewa, mkoani Njombe.

MBUNGE ATAKA KISWAHILI KITUMIKA HADI VYUO VIKUU


MBUNGE wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM), amehoji lini serikali itapitisha Kiswahili kitumike kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu. Aidha, alisema mwaka 2004, Umoja wa Afrika ulipitisha Kiswahili kiwe ni lugha ambayo itatumika katika mikutano na shughuli mbalimbali.

“Je, serikali imejiandaa vipi kupeleka wakalimani wa kutosha kutoka Tanzania ili waweze kujipatia ajira?” alihoji.


Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala alisema jitihada zinafanywa na taasisi hizo za kukuza Kiswahili mojawapo kuandika vitabu vingi vya kufundishia na kuongeza wataalamu.

“Nasema wazo hilo tumelipokea na sisi ndani ya serikali tunaendelea kulifanyia kazi na hata wakati tunawasilisha bajeti yetu zilitoka hoja hizo za kuwa Kiswahili kifundishwe madarasani,” alisema.

Aidha, Makala alikiri kupitishwa kwa azimio hilo na kuongeza kuwa:

“Kama Tanzania tumeona kuwa hii ni fursa muhimu na tayari moja ya kazi zinazofanywa na Taasisi za kukuza Kiswahili, BAKITA, BAKIZA ni kuongeza wataalamu zaidi ili waweze kupata ajira hiyo.”


Aliongeza kuwa Tanzania kama Tanzania mjini Addis Ababa kuna kituo cha kufundishia lugha ya Kiswahili. Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine (CCM) alitaka kufahamu kama nchini Tanzania kuna Sera ya Lugha.

Pia, alihoji kama ipo, je, sera hiyo ya Lugha imeipatia hadhi gani lugha ya Kiswahili.


Aidha, alitaka kujua kuna mkakati gani mahsusi wa kuifanya Lugha ya Kiswahili kuwa ya kufundishia kwa viwango vyote vya elimu hapa nchini.

Akijibu swali hilo, Makala alisema Tanzania hakuna andiko mahususi au linalosimama pekee kama Sera ya Lugha, bali suala la lugha limezingatiwa kama Sura maalumu muhimu ndani ya Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997.


Alisema katika andiko hilo la sera ya Utamaduni, Kiswahili kimetambuliwa kuwa siyo tu lugha ya mawasiliano mapana nchini bali pia ni lugha ya taifa na mojawapo ya lugha rasmi mbili za Taifa.


Aidha, alisema miongoni mwa mikakati mahsusi ya kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ni jitihada zinazoendelea za wataalamu wa Asasi za ukuzaji wa Kiswahili nchini ambazo ni kuboresha sarufi ya Kiswahili, kutunga Kamusi za Kiswahili za masomo na taaluma mbalimbali.

Tuesday, 4 June 2013

MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWAIR KUWASILI LEO SAA NANE MCHANA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Albert Mangweha tunapenda kuwaatarifu rasmi kuwa mwili wa marehemu Ndugu yetu, mpendwa wetu Albert Mangweha utawasili [leo] tarehe 04/06/2013 saa nane mchana na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Terminal One).

Tunaomba mjitokeze kwa wingi kwa ajili ya kumpokea ndugu yetu, mpendwa wetu Albert Mangweha.

Taarifa hii kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mapokezi na Mazishi. Asanteni na Mungu awabariki.

TANZANIA SASA KUONGOZWA NA MARAIS WATATU, MGOMBEA BINAFSI RUKSA...



Rasimu ya Katiba imetolewa na Tume ya marekebisho ya katiba na miongoni mwa mambo yanayopendekezwa ni kuundwa kwa Serikali tatu pamoja na kuruhusiwa kwa mgombea binafsi. 

Uzinduzi wa rasimu hiyo ya katiba umefanyika jana, Dar es Salaam na kwa uamuzi huo wa tume sasa Tanzania itakuwa na marais watatu ambao ni rais wa serikali ya shirikisho, rais wa Tanzania Bara na rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Alisema tume yake inapendekeza serikali tatu, kwani wananchi ambao walitoa mapendekezo hayo ni wengi kuliko makundi ya waliotaka serikali moja, serikali nne, muungano wa mkataba na serikali mbili.

"Sababu zao zilikuwa nzito lakini pia kulikuwa na changamoto nyingi na nzito. Pamoja na maoni ya wananchi, tume ilirejea sababu za kupendekeza muundo huu zilizotolewa na tume zilizopita na tafiti zilizofanywa na tume kuhusu aina mbalimbali za muungano," alisema Warioba.

Alisema pamoja na maoni ya wananchi, tume ilirejea sababu za kupendekeza muundo huo zilizotolewa na tume zilizopita na tafiti zilizofanywa na tume kuhusu aina mbalimbali za muungano.

"Baada ya yote hayo tume hatukuwa na jinsi zaidi ya kufikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa serikali tatu, yaani serikali ya shirikisho, serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar," alisema Warioba.

Hivyo kutakuwa na serikali ya muungano, serikali ya Tanzania Bara, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Shughuli za Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa na serikali ya muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano na mahakama yake.

Kutokana na uamuzi huo wa tume, muundo, madaraka na mambo mengine ya kiuendaji yahusuyo serikali ya Bara na ile ya Zanzibar yataainishwa katika katiba za washirika hao wa muungano.

Katika rasimu hiyo serikali ya muungano itakuwa ndio chombo chenye mamlaka ya utendaji, Bunge litakuwa na mamlaka ya kutunga sheria kwa mambo ya muungano na mahakama kitakuwa chombo cha kutoa haki katika muungano huo.

Kwa mujibu wa rasimu hiyo, serikali ya Bara itakuwa na mamlaka juu ya mambo yasiyo ya muungano yanayohusu eneo hilo na SMZ, pia itakuwa na mamlaka ya juu yasiyo ya muungano yaliyoko eneo lake. “Washirika wa muungano watakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya muungano na watatekeleza."

Washirika hao wanaruhusiwa kuanzisha mahusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo yaliyo chini yake kwa mujibu wa katiba yake. 

Katika eneo hilo inapendekezwa kuwa mshirika wa muungano anaweza wakati wa kutekeleza majukumu yake kuomba ushirikiano kutoka serikali ya muungano kwa ajili ya kufanikisha uhusiano na jumuiya au taasisi za kimataifa au kikanda na serikali ya muungano inaweza kutoa ushirikiano kwa mshirika huyo kwa namna itakavyohitajika.

Inapendekezwa kila mshirika wa muungano atateua waziri mkazi atakayeratibu na kusimamia uhusiano baina ya serikali za washirika na kati ya serikali ya mshirika na serikali ya muungano, mawaziri hao wakaazi watafanya kazi zao na ofisi zao zitakuwa makao makuu ya serikali ya muungano na watakuwa kiungo kati ya serikali ya muungano na serikali mshirika

Tume hiyo pia imepunguza mambo ya muungano kutoka 22 hadi saba ambayo ni katiba na mamlaka ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ulinzi na usalama wa Jamhuri, uraia na uhamiaji, sarafu na benki kuu, mambo ya nje, usajili wa vyama vya siasa, ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya muungano.

Katika muundo huo serikali ya muungano itapata mamlaka yake kutoka kwa wananchi wa pande zote na serikali za serikali washirika nazo zitachaguliwa na wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaosimamiwa na tume za uchaguzi za nchi zao. Viongozi wote hao wanalazimishwa na katiba hiyo kulinda na kuimarisha muungano.
Jaji Joseph Warioba alisema tume yake imezingatia maoni ya wananchi ambao walipendekeza haki zote ziimarishwe na kusiwe na vikwazo vya lazima.

Kutokana na maoni hayo, Warioba alisema tume yake inapendekeza kwamba vikwazo vilivyowekwa kuzuia mgombea huru viondolewe, kwa maana nyingine tume inapendekeza mgombea binafsi aruhusiwe.

Kwenye rasimu hiyo ya katiba, pia haki mpya zimeingizwa ambazo ni haki ya mtoto, haki za watu wenye ulemavu, haki za wanawake, haki za wazee, haki za makundi madogo katika jamii, haki ya elimu na kujifunza, haki ya kupata habari, haki na uhuru wa habari na vyombo vya habari.

Rais wa shirikisho ndiye atakayekuwa amiri jeshi mkuu na yeye atakuwa na makamu mmoja. Rais huyo atakuwa ndiye taswira ya Muungano wa Tanzania. Pia kutakuwa na bunge la muungano, na mahakama ya Muungano.

Makamu wa Rais ndiye atakayekuwa msaidizi mkuu wa Rais.
Tume hiyo imependekeza umri wa kugombea urais uendelee kuwa miaka 40 kwa vile idadi kubwa ya watu waliotoa maoni walipendekeza umri huo.

Kwenye mapendekezo hayo, Warioba alisema mgombea wa nafasi ya rais atatangazwa kuwa mshindi iwapo atakuwa amepata kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa.

Inapendekezwa kuwa uchaguzi wa rais itakuwa kama ilivyo sasa isipokuwa tume hiyo imependekeza mgombea urais aweza kupendekezwa na chama cha siasa au kuwa mgombea huru.

Katika rasimu hiyo tume hiyo imependekeza kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kulalamikiwa mahakamani. 'lakini sio kila mtu anaweza kufungua kesi, wanaoweza kufungua kesi ni wagombea urais.'

Pia tume hiyo imependekezwa kuundwa kwa mahakama ya juu (supreme court) ambako wagombea urais wanaweza kufungua kesi na ni mahakama hiyo tu itakuwa na mamlaka na uwezo wa kusikiliza malalamiko kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais na shauri lazima liamuliwe ndani ya siku thelathini.

"Rais aliyeshinda ataapishwa siku 30 tangu alipotangazwa kuwa mshindi au kuthibitishwa na mahakama," alisema Warioba.

Warioba alisema katika eneo hilo tume imependekeza rais abaki na madaraka ya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu. Lakini imependekezwa rais ashirikiane na taasisi na vyombo vingine katika uteuzi huo.

Alisema uteuzi wa mawaziri na manaibu waziri Rais atateua na Bunge lithibitishe, lakini kuhusu jaji mkuu na naibu jaji mkuu ambaye tume imependekeza cheo hicho kiwepo, majina ya watu waliopendekezwa na tume ya utumishi wa mahakama na baada ya hao bunge litathibitisha. Kwa upande wa makatibu wakuu watateuliwa na rais kutokana na mapendekezo ya tume ya utumishi wa umma.

Kwa upande wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, inapendekezwa kuwa kianzishwe chombo kipya kitakachoitwa baraza la ulinzi na usalama wa taifa ambalo kati ya majukumu yake itakuwa ni kumshauri rais kuhusu uteuzi wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Kinga ya rais imependekezwa na tume hiyo ibaki na anaweza kushtakiwa na Bunge kama ilivyo katiba ya sasa.

Katika mapendekezo hayo imependekezwa kuwa rais aunde serikali ndogo iliyo na mawaziri wasiozidi 15 na mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hao hawatahudhuria vikao vya Bunge isipokuwa watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.

Kwa upande wa Bunge, Warioba alisema inapendekezwa wabunge wa aina mbili. Yaani kutakuwa na wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wachache wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha watu wenye ulemavu. Tume imependekeza mbunge akifukuzwa na chama cha siasa abaki kuwa mbunge lakini akihama chama atapoteza ubunge wake.

Katika eneo hilo pia rasimu inapendekeza kuwepo ukomo wa ubunge ambao ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano lakini wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wa kipindi iwapo hawaridhiki na utendaji wake wa kazi.

Pia imependekezwa kusiwepo na uchaguzi mdogo isipokuwa kama nafasi inayokuwa wazi inatokana na mbunge huru ndipo uchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo utafanyika, "lakini kama nafasi ikiwa wazi kutokana na mbunge wa chama cha siasa basi nafasi hiyo ijazwe na mtu kutoka chama hicho.”

Kwa upande wa spika na naibu spika, inapendekezwa wasitokane na wabunge na wasiwe viongozi wa vyama vya siasa.

Jaji Warioba alisema tume yake imefanya uchambuzi wa maoni ya wananchi katika eneo hilo na imependekeza jina la tume liwe Tume Huru ya Uchaguzi. Tume pia imependekeza sifa za wajumbe wa tume hiyo huru ziwekwe kwenye katiba na watapatikana kutokana miongoni mwa watu wenye sifa zilizoainishwa ndani ya katiba kwa kuomba.

Alisema majina ya waombaji yatachambuliwa na kamati ya uteuzi ambayo mwenyekiti wake atakuwa jaji mkuu na wajumbe wengine sita ambao ni majaji wakuu wa nchi washirika, spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano na maspika wa mabunge ya nchi washirika na mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu.

Alisema kamati hiyo itapendekeza majina ya watu wnaofaa kwa rais ambaye atateua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wengine.

"Bunge litathibitisha uteuzi wao, wabunge na viongozi wengine wa kisiasa hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe wa tume ya uchaguzi."

Katika eneo hilo imependekezwa kuwa tume huru ya uchaguzi isimamie masuala ya uchaguzi, kura ya maoni na usajili wa vyama vya siasa.

Kuhusu mahakama imependekezwa kuwa majaji wa mahakama ya juu (supreme court) na mahakama ya rufaa watateuliwa na rais baada ya kupendekezwa na tume ya utumishi wa mahakama.

Kwa kuwa tume imependekea muungano wa shirikisho, kutokana na uzito wa maoni ya wananchi, hivyo kutakuwa na benki kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayokuwa na wajibu wa kusimamia masuala ya sarafu na fedha za kigeni na benki za washirika wa muungano.

Pia inapendekezwa kuwepo na benki zitakazokuwa na jukumu la kutunza akaunti ya fedha za serikali za kila mshirika wa Muungano na kuzisimamia benki za biashara katika mamlaka zao.

Katiba inapendekeza makamu wa rais atatoka upande mwingine wa muungano ambako hatoki rais wa muungano.

Mgombea binafsi anaruhusiwa kumteua makamu wa rais hata kama mtu huyo alishashika wadhifa wa urais wa Zanzibar au wa Tanzania bara. Ikitokea rais wa bara au wa SMZ akateuliwa kuwa makamu wa rais atalazimika kuacha wadhifa wake wa awali ili ashike wadhifa huo wa juu katika Jamhuri.

Kwa muundo huo baraza la mawaziri sasa litaundwa na makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano, mawaziri wa serikali ya muungano, mwanasheria mkuu wa serikali atahudhuria vikao vya baraza hilo lakini hatakuwa na haki ya kupiga kura.

Baraza hilo la mawaziri ndilo litamshauri rais na bunge na mahakama havitakuwa na uwezo wa kuchunguza jambo ambalo limepitishwa na baraza la mawaziri.

Katiba iliyopendekezwa ina ibara 20 kutoka za sasa ambazo ni 153. Misingi mikuu ya taifa iliyoko kwenye katiba hiyo ni saba kutoka minne ya awali ambayo ni uhuru, haki, udugu, usawa, umoja, amani na mshikamano.

Tunu za taifa katika katiba hiyo ni utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji, na kiswahili.

Kwenye katiba hiyo pia kuna malengo ya taifa ambayo yatakuwa ni mwongozo kwa serikali, bunge, mahakama, vyama vya siasa, taasisi na mamlaka nyingine kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya katiba au sheria nyingine za nchi.

Kwa msingi huo, tume hiyo imependekeza malengo makuu ya taifa yapanuliwe kwa mpango wa kuonyesha malengo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutumaduni, kimazingira, na sera ya mambo ya nje.

Vyombo vya kikatiba katika rasimu hiyo ni tume ya uhusiano na uratibu wa serikali, baraza la mawaziri, kamati maalum ya makatibu wakuu na sekretarieti ya baraza la mawaziri, baraza la ulinzi na usalama la taifa, tume huru ya uchaguzi, tume ya utumishi wa mahakama, tume ya utumishi wa umma, tume ya maadili ya viongozi na uwajibikaji na tume ya haki za binadamu na utawala bora.

Katika katiba hiyo inapendekezwa kuwa maadili ya viongozi wa umma pamoja na miiko ya uongozi yawekwe kwenye katiba na tume imependekeza sekretarieti ya maadili ibadilishwe kuw atume yenye mamlaka makubwa ya kusimamia maadili ya viongozi wanaovunja miiko ya uongozi.

Monday, 3 June 2013

BABA MZAZI WA MWISHO MWAMPAMBA ARUDISHA KADI YA CHADEMA NA KUCHUKUA YA CCM!!


Baba mzazi mzee Mwampamba akirudisha kadi ya chadema mbele ya Jemedari Mwigulu Nchemba nyumbani mlowo morogoro......

Monday, 27 May 2013

SASA MAKETE KAZI IMEANZA:: TAZAMA VIFUSI BARABARA ZA MITAA MAKETE MJINI VIKISAMBAZWA

Kazi ikiwa inaendelea kama kawaida (Picha na EMB)

Sunday, 26 May 2013

BAADA YA PICHA ZA AJABU NA AIBU SASA THE COMEDY KUSHITAKIWA MAHAKAMANI!!


Zile picha za kundi la Ze Komedy la linalorusha kipindi chake kupitia televisheni ya East Africa TV zinazowaonesha wasanii hao wakiwa na mabint ufukweni zimechukua sura mpya baada ya wanasheria  kuahidi kuzisaidia familia za wazaza wa mabint hao.

Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema" Nimeziona picha hizo kupitia mtandao wenu kweli imeniuma kama mzazi kwani huo ni unyanyasaji ambao haukubariki hata kidogo naziomba familia za mabint hao kuchukuwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kushtaki ili iwe fundisho kwa wasanii wengine wanaopenda kudhalilisha watu wengine kwa masrahi yao binafsi" Alisema Fortunatus Kasomfi ambae ni mtanzania anaeishi nchini Afrika Kusini

Aidha nae Hawamu Juma ambae ni mkazi wa Arusha maeneo ya Unga Limited ambae ni Mwanasheria maarufu Mkoani humo alioneshwa kusikitishwa sana na tukio na kuwashauri wazazi wa wasichana hao kumtafuta kwa ajili ya kuwafungulia mashtaka wasanii hao
 
" Napenda kuwashauri wazazi wa wabinti hao kama wanahitaji msaada wa kisheria wanitafute kupitia  simu namba 0713-146416 nitawapa mawazo ya kitaalam ya kisheria ili wasanii hao wafikishwe mahakamani" Alisema Mwanasheria huyo

Taarifa  za  ndani ya chungu zinadai  kuwa  kulikuwa na ushawishwaji mkubwa kwa mabinti hao wakati wa kupigana picha hizo kwa madai kuwa watasaidiwa kuwa mastaa kama watapiga picha hizo na mastaa hao. 
 
Huyu  ni  Happy na Master  Face  wakifanya  Uchafu wao....Hapa  wanatomasana  kabla ya uzalendo kuwashinda  na  kuamua  kuvunja  amri  ya  sita...


 
Tayari kuna taarifa kuwa baba mzazi wa mmoja wa wasichana hao ambae anaishi Tabata ameanza kuchukuwa hatua za awali kwani siku ya tukio msanii wa kundi la Komedy Manaiki Sanga alifika nyumbani kwa bint huyo na kumchukuwa kwa madai kuwa anaenda nae Location.

Mpaka sasa kiongozi wa kundi hilo ambaye  ni Mtanga ameshindwa kuchukuwa hatua yoyote dhidi ya wasanii wake walihusika na tukio hilo chafu ....

VIKONGWE WATATU WAUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO HUKO BUNDA


MAUAJI ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja kama Kuku kisha kuwachoma moto vikongwe watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha na vitendo vya kishirikina. 

 Pia watu hao mbali na kuwaua kikatili vikongwe hao kwa tuhuma kwamba walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa wakiwafuga na kuwatafuna kumaliza hasira zao.

 Kwa mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa, tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye hasira kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua kijana huyo hivi karibuni.
 

Kijana huyo alikufa kwa kugongwa na gari, lakini dereva aliyemgonga alidai hakuona kama alimgonga mtu ila mbwa na pia inaelezwa  tangu azikwe kijana huyo alikuwa akirejea kwa mkewe na kumuita nyakati za usiku pamoja na kusumbua familia yao akitaka apewe chakula na ndipo wanafamilia hao walipoamua kwenda kwa mganga kuchunguza tukio hilo. 

Wakiwa kwa mganga,wanafamilia hao walitajiwa majina ya wanakijiji watatu wa kijiji hicho ambao hata hivyo walitoroka kwenda vijiji vya jirani pamoja na familia zao kabla ya usiku wa leo kuvamiwa walipokuwepo na kuangushiwa adhabu hizo za kinyama. 

Wa kwanza kushambuliwa na kuuwa ni bibi aitwaye Bi Mgala ambaye alikimbilia kijiji cha jiorani kwa rafiki yake aitwaye Bi Laya, ambapo walimkata miguu yote miwili na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili kabla ya kumchoma moto ambapo hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba ziliungua nguo zake tu huku mwili ukiwa upo vile vile. 

Baadaye walimgeukia Bi Laya aliyekuwa akitaka kuwatoroka na kumfanyia unyama kama rafikie kwa kosa la kumhifadhi Bi Mgala kwa kuamini huenda wanafanya shughuli za kishirikina pamoja na baadaye kurudi Kasaula na kumnasa Bi Chausiku na kumfanyia kama walivyowafanyia ajuza hao wengine kisha kuchoma nyumba tatu. 

 Bibi wa tatu wanayemtuhumu pia kwa ushirikina, ametimka kijijini hapo, lakini nyumba yake imeteketezwa pamoja na kuku waliokuwa wakiwafuga kuporwa na watu hao na kutumia moto waliouwasha katika nyumba hizo kuwachoma na kuwala kwa hasira. 

Kamanda wa Polisi wa Bunda, Mika David Nyange amethibitisha juu ya tukio hilo la kusikitisha na kwamba wanedelea na upelelezi kwa nia ya kuwasaka waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mikononi.

Tuesday, 21 May 2013

RAIS KIKWETE AMWAGIA SIFA LOWASSA......AMEDAI KWAMBA LOWASSA NI "JEMBE"


Rais Jakaya Kikwete amemwagia sifa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa hatua ambayo inaweza kutafsiri mengi katika medani ya siasa nchini.
 
 Akizungumza na wabunge wa CCM kwenye Ukumbi wa White House Dodoma juzi, Rais Kikwete ambaye pia mwenyekiti wa chama hicho, alisema nguvu za Lowassa pekee zinatosha kushinda uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani Kata ya Makuyuni kilichoko wilayani Monduli.

Kata ya Makuyuni iko wilayani Monduli, ambako Lowassa amekuwa mbunge wake tangu mwaka 1995.

Habari za kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kuhusu kampeni za uchaguzi huo wa Makuyuni, baada ya kuwa ametoa ruksa kwa makada wa chama hicho wanaotaka urais kuanza kujipitisha pitisha miongoni mwa wanachama wa chama hicho. 

Lowassa anatajwa kuwa miongoni mwa wanaCCM wanaotaka kumrithi Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

“Sina tatizo na pale Makuyuni, najua muscles (misuli) za Mzee Lowassa zinatosha kutupa ushindi; au vipi mzee?” alidokeza mmoja wa wabunge wa CCM akimnukuu Rais Kikwete.

Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Makuyuni unaotarajiwa kufanyika Juni 16, mwaka huu, utakuwa wa ushindani mkali kati ya CCM na Chadema ambao historia yao kisiasa mkoani Arusha ni ya uhasama.

Katika uchaguzi huo, unaofanyika baada ya kifo cha Abdillah Warsama (CCM), chama hicho kitatetea nafasi yake kwa kumsimamisha Godluck Lerunya na Chadema ni Japhet Sironga. 

Mbali na Kata ya Makuyuni, uchaguzi wa udiwani mkoani Arusha utafanyika pia katika Kata za Kaloleni, Themi, Kimandolu na Elerai, kutokana na waliokuwa madiwani wa kata hizo (Chadema), kufukuzwa na chama chao.

“Mnaweza kuchafuana leo, kesho mkapata mgombea mwenye nundu nyingi na mabandeji kila mahala, halafu mkapata shida kumnadi,” alisema.

Siyo mara ya kwanza kwa Kikwete kumsifia Lowassa kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka jana huko Longido wakati akikabidhi ng’ombe.
 
Pia aliwahi kumsifia wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 wakati Kikwete alipomwelezea Lowassa kama Mbunge makini na kuwaomba watu wa Monduli kumchagua tena.

Hata hivyo, alipoulizwa kama baada ya kuruhusiwa kuanza kujipitisha kwa wanaCCM kama anataka kuwania urais, Lowassa alijibu kupitia watu wake wa karibuni kuwa asingependa kuzungumzia suala hilo hasa baada ya Rais kutoa kauli hiyo.

Kutangaza nia ruksa

Rais Kikwete aliwaeleza wabunge hao kuwa si kosa kwa watu kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwamo urais mwaka 2015.

“Wabunge na mawaziri wenye nia ya kutangaza nia ya kugombea urais wawe huru, kwani hiyo ni haki yao, isipokuwa wafanye kwa wema bila kukivuruga chama na kuwagawa wanaCCM katika makundi. Sioni tatizo watu kujipitisha. Sisi sote hapa tulijipitisha. Lakini tufanye hivyo kistaarabu bila kuvurugana.”'

Aliwaagiza wabunge wa chama hicho kwenda majimboni mwao kusikiliza kero za wananchi badala ya kusubiri wakati wa uchaguzi.

Kauli ya Membe

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye naye anatajwa kuwa miongoni mwa wagombea amewataka waandishi waache kuandika kila siku habari za urais na badala yake waandike mambo ya maendeleo. 


Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kukutana na mabalozi wa nchi zinazoendelea kuhusu Mkutano wa Smart Partnership, unaotarajiwa kufanyika nchini, Membe alisema ni vizuri yakaandikwa mambo ya maendeleo na si kila wakati kuandika mambo ya urais.

“Mkutano kama huu nchi kama Kenya watauripoti vizuri na kwa undani hivyo mfanye hivyo si kila kitu urais 2015,” alisema Membe.

 Mkutano huo utaanza Mei 28, hadi Juni Mosi na utajadili jinsi gani sayansi na teknolojia vinaweza kutumika kuzikwamua kiuchumi.


CHANZO: MWANANCHI

Monday, 20 May 2013

TASWIRA ZA DC MAKETE AKISOMA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI MAKETE JANA HAPA ANGALIA

Mkuu wa wilaya ya makete Mh. Josephine Matiro akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali wilayani hapo kwa kipindi cha Januari-Aprili 2013 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete jana Mei 20,2013
Hapa Mh. Matiro akitilia mkazo kuhusu wanafunzi wote kupata chakula mashuleni
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya makete Bw. Idd Nganya akijibu hoja katika kikao hicho
Afisa elimu msingi wilaya ya Makete Antony Mpiluka akitoa msisitizo kuhusu wanafunzi kupatiwa chakula shuleni
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya makete Francis Chaula akichangia jambo katika kikao hicho
Afisa maliasili na Mazingira wilaya ya Makete Bw. Uhuru Mwembe akijibu hoja za idara yake ambazo zimeulizwa na wajumbe
katibu wa CUF wilaya ya Makete Bw. Joma Mwakisitu akiuliza swali
Msaidizi wa askofu KKKT dayosisi ya kusini kati Mch. Philemon Kahuka akiuliza maswali hsa kuhusu maji makete mjini 
Katibu wa CCM wilaya ya makete Bw. Miraji Mtaturu akizungumza kuhusu barabara na mfuko wa jamii CHF
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya makete Shaaban Mkakanze akichangia hoja kikaoni hapo
Mzee Masevela naye hakuwa nyuma kuchangia
Mwakilishi wa NMB Makete akizungumza
Mhandisi wa ujenzi wilaya Makete Eng. Samwel Ndoveni akijibu hoja za idara yake hasa usambazaji wa vifusi makete mjini ambapo amesema kazi itaanza leo
Kaimu mganga mkuu wilaya ya makete Dk. Alexander akijibu hoja za idara ya afya
Afisa mtendajia kata ya Iwawa Festo Msigwa akishiriki kuchangia hoja
Washiriki wakifuatilia mambo

BABA MZAZI AJINYONGA BAADA YA MWANAE KUFA AKITOA MIMBA WILAYANI LUDEWA MKOANI NJOMBE

 
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Ngonyani
 
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Matema wilayani Ludewa mkoani Njombe amefariki Dunia Baada ya kushindikana kwa jaribio la kutoa mimba Nyumbani Kwa Mganga wa Zahanati ya Kijiji Cha Lifuma. 
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Acp Fulgency Ngonyani amethibitisha kutokea kwa matukio hayo wilayani Ludewa.
 
Kamanda  Ngonyani amemtaja Binti huyo kuwa ni Grace Mwakila alieyefariki Dunia wakati akiwa nyumbani kwa mganga wa Zahanati hiyo wakati akijaribu kutoa mimba.

Amesema kuwa tukio hilo limetokea may 16 mwaka huu majira ya saa tisa alfajiri katika kijiji cha Lifuma ambapo mganga wa kituo cha afya Lifuma Dkt.Michael Nkoma alijaribu kumtoa mimba binti huyo na kumsababishia mauti.

Kamanda Ngonyani amesema kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi linamshikilia Mganga huyo aliyemtaja kwa jina la Michael Mkoma kwa mahojiano zaidi.
 
Taarifa zilizotufikia daktari huyo alipofanya jaribio la utoaji mimba na baada ya kushindwa na kumsababishia mauti manafunzi huyo alikaa na mwili wa mwanafunzi Grace ndani mwake kwa siku mbili ndipo alipoamua kutoa taarifa katika uongozi wa kijiji cha Lifuma kwa kuomba usalama wake.
 
Baba mzazi wa binti aliyekufa kwa kutoa mimba Bw.Longinusi Mwakila amefariki dunia kwa kujinyonga na kamba ya Manila kufuatia kufariki kwa binti yake baada ya Kutoa Mimba.
 
Wananchi wa kijiji cha kilondo ambao hawakutaka majina yao yatajwe walisema kutokana na upendo wa Baba mzazi wa binti huyo kwa mwanae nae aliamua kujinyonga ili asishuhudie mazishi yamwanae aliyempenda.

Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya kujinyonga mkoani Njombe katika Kipindi cha mwezi mmoja na hivyo jeshi la Polisi kuwataka wananchi kutambua kuwa utoaji ni mimba ni kosa la Jinai ambalo ni hatari katika maisha Yao.
 
Hata hivyo baadhi ya ndugu wa marehemu hao wamelilalamikia jeshi la Polisi wilayani Ludewa kwa kutompeleka mtuhumiwa huyo mapema mahakani na kukaa nae kwa muda wa siku tano katika kituo cha polisi.
 
Na Nickson Mahundi