MTALIANO Mario Balotelli amefunga mabao mawili usiku huu ikiwemo penalti babu kubwa, akiiwezesha AC Milan kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Pescara mabao 4-0.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City alifunga bao lake la kwanza kwa penalti kabla ya kufunga lingine katika mechi ambayo wachezaji wengine waliowahi kucheza Ligi Kuu ya England Sulley Muntari na Mathieu Flamini walifunga.
Amekuwa na mafanikio tangu arejee Italia na Milan wamekuwa hawafungwi katika mechi ambazo anacheza Serie A, ikishinda nane na kutoa sare tatu.
Mario Balotelli akifunga kwa mkwaju wa penalti
Balotelli akishangilia na Robinho
Waliocheza England wanatisha: Sulley Muntari akishangilia bao lake
Balotelli akimtoka Marco Capuano
Wachezaji wa Milan wakishangilia