WAKATI Sir Alex Ferguson anaachia ngazi, mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney ameomba kuondoka pia Old Trafford wakati ambao habari zinasema klabu iko mbioni kumrejesha Cristiano Ronaldo.
Saa kadhaa baada ya Ferguson kuthibitisha atastaafu ukocha United mwishoni mwa msimu, akimpisha kocha wa Everton, David Moyes, inabainika Rooney alimuambia Ferguson wiki mbili zilizopita anataka kuanza maisha mapya.
Wakati huo huo, inagundulika, Mtendaji Mkuu wa United, David Gill alikuwa mjini Madrid kukutana na Jorge Mendes, wakala maarufu Mreno anayemuwakilisha Ronaldo.
Vyanzo vimesema jana usiku kwamba, United inajiamini itamrejesha mchezaji huyo iliyemuuza Real Madrid kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 80, mwaka 2009.
Jinsi walivyokuwa: Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo wakati wanacheza pamoja Manchester United
Katika bluu: Chelsea ina matumaini ya kumnasa mshambuliaji huyo wa England kwa Pauni Milioni 25 ahamie Stamford Bridge msimu ujao