
Muwakilishi kutoka benki ya NMB akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya TANESCO,mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group na kufanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Bonaza hilo lilijumuisha makampuni 14 na yote yalichuana vikali kuhakikisha kila mmoja anajitahidi kushinda ili kulinda heshima.Lengo la la bonanza hilo ilikuwa ni kuwaweka pamoja wafanyakazi wa kampuni mbalimbali ili waweze kufahamiana na pia kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao.




