Wednesday, 8 May 2013

MBOWE AWAONGOZA VIONGOZI WA CHADEMA KUTOA POLE KWA WAHANGA WA BOMU KANISANI ARUSH

 Mbunge wa arumeru mashariki-chadema Joshua Nasari(kushot)akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mhe Freeman Mbowe muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa arusha kwa ajili ya kuwapa  pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mt Meru kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi, katika parokia teule ya Olasiti, Arusha, lililotokea Jumapili iliyopita, Mei 5, 2013 Kulia kwake ni mbunge wa arusha mjini-Chadema Godbless Lema
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mhe Freeman Mbowe akisalimiana na watu mbalimbali muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa arusha kwa ajili ya kuwapa  pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mt Meru kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi, katika parokia teule ya Olasiti, Arusha, lililotokea Jumapili iliypoita, Mei 5, 2013
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mhe Freeman Mbowe akiongea na waaandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa arusha kwa ajili ya kuwapa  pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mt Meru kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi, katika parokia teule ya Olasiti, Arusha, lililotokea Jumapili iliypoita, Mei 5, 2013.kushoto kwake niMbunge wa arumeru mashariki-chadema Joshua Nasari na Kulia ni Kulia kwake ni mbunge wa arusha mjini-Chadema Godbless Lema.Picha na Chadema
 

Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mhe Freeman Mbowe jana jioni aliwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mt Meru kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi, katika parokia teule ya Olasiti, Arusha, lililotokea Jumapili iliypoita, Mei 5, 2013.
 
Baadaye katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, Mbowe aliwapa pole wote walioathirika kwa janga hilo kwa namna yoyote, na kuwataka Watanzania wote wawe watulivu wakati vyombo vya dola vinafanya kazi yake, lengo likiwa ni kuwapata wahusika ili ijulikane hasa lengo lao. 

 Baada ya kutoka hopsitalini, Mbowe na msafara wake walielekea Elerai kuhani msiba mmoja wa waliofariki.

Mbowe katika msafara wake aliambatana na wabunge wa chama hicho kwa majimbo ya Arusha Mjini na Arumeru Mashariki, pamoja na viongozi wa juu wa Chama wa Kanda ya Kaskazini.