KLABU ya Galatasaray imetwaa taji la 19 la ubingwa wa Ligi Kuu ya Uturuki, baada ya kuifunga Sivasspor mabao 4-2 mjini Istanbul.
Mabao mawili kila mtu ya Selcuk Inan na Burak Yilmaz yaliipa timu ya Fatih Terim ushindi dhidi ya Sivasspor, ambayo mabao yake yalifungwa na Kadir Bekmezci na Cihan Ozkara.
Ushindi huo, unafuatia kipigo cha Fenerbahce cha mabao 2-0 kutoka kwa Istanbul BB, ambao sasa wanazidiwa mara moja idadi ya kutwaa mara nyingi ubingwa nchi hiyo, kwani wao wametwaa mara 18.
Aidha, ushindi huo unamfanya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba atwae taji lingine katika nchi nyingine.
Mabingwa kwa pointi 10 zaidi kileleni zikiwa zimebaki mechi mbili
Drogba alicheza tangu mwanzo hadi mwisho, lakini kiungo Wesley Sneijder, aliyesajiliwa kutoka Inter Milan ambaye kama ametwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, alicheza saa moja tu.
Nyota Yilmaz, amefikisha mabao 21 msimu huu, na sasa Galatasaray inaongoza ligi kwa pointi 10 zaidi zikiwa zimebaki mechi mbili.
Wapinzani wao wakubwa, Fenerbahce wametwaa mataji 18
Kipenzi cha mashabiki: Didier Drogba ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Galatasaray
Kocha Terim Terim alifungiwa mechi tisa Aprili kwa kumbwatukia refa katika mechi ya ligi dhidi ya Mersin Idmanyurdu na hakuwepo kwenye benchi timu yake ikisherehekea ushindi huu kwa kutumikia adhabu yake.
Mzee wa mipango: Fatih Terim ni kocha wa Galatasaray
Anayelengwa: Drogba bado anaokota mafanikio Ulaya