Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 wa Atletico Madrid amekuwa gumzo kuelekea dirisha la usajili, akiwaniwa na klabu kadhaa zikiwemo Chelsea na Manchester City pia.
Lakini mshambuliaji wa zamani wa Newcastle, Asprilla anaamini nyota huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 46 anaweza kutua Old Trafford msimu ujao.
Atapendezaje? Fikiria vipi Radamel Falcao ataonekana katika jezi ya Manchester United
Anawaniwa: Radamel Falcao
Asprilla amesema: "Tulizungumza na aliniuliza mimi maoni yangu aende timu gani. Anafahamu kwamba kila klabu kubwa duniani inamtaka. Ni mchezaji asiyehadaika na fedha - anachotaka ni sehemu ambayo familia yake itafurahia na ambako atapata mafanikio.
"Na timu kama Real Madrid, PSG, Manchester City zina wakati mzuri kuliko zinavyokuwa na wakati mbaya - na ndiyo maana nikamuambia lazima achague Manchester United. Kila msimu wanapigana - na ikiwa anataka mafanikio huko ndiko ambako nimemuambia aende.
Asprilla anaamini Falcao atakuwa mchezaji pekee daima kucheza Ligi Kuu ya England ambaye anaweza kufanya vitu kama Alan Shearer.
"Ni vigumu kwangu kufafanua ni mzuri kiasi gani - ni mmaliziaji mzuri zaidi duniani. Mchezaji pekee aliyecheza Ligi Kuu England ambaye ana kiwango chake cha umaliziaji ni Alan Shearer.
"Ikiwa atasaini Manchester United - atawasaidia kupata taji la Ligi ya Mabingwa. Robin van Persie na Radamel watakuwa hawakamatiki,".
Muuwaji: Falcao amekuwa hakamatiki anapokuwa mbele ya mdomo wa lango Atletico Madrid
VIDEO: Mabao ya Falcao... Mabao lukuki