Mwanamuziki aliyeitikisa vilivyo Kenya kabla ya kuokoka na kuachana na muziki wa kidunia, mwanadada Size 8 sasa ameanza kufunguka katika interview kwenye vituo mbali mbali vya redio na Tv kuhusiana na maisha mapya ya kidini.
Kati ya yote ambayo Size 8 amekuwa akiyaongelea, ni moja tu ambalo amekuwa akilitilia mkazo kwa kumaanisha kuwa linamsikitisha zaidi ni suala lake la kupoteza BIKRA, Size 8 amewaambia watu kuwa "Najutia sana kupoteza bikra yangu. Ninaamini kuwa kijana anatakiwa kujilinda na kujizuia kufanya ngono katika ujana wake wote mpaka atakapo pata kibali toka kwa Mungu."