BONDIA Muingereza Amir Khan amedhihirisha kwamba 'yeye mzima' baada ya kumudu kushinda kwa pointi pambano ambalo alidondoshwa chini katika raundi ya nne dhidi ya Julio Diaz wa Mexico jana usiku.
Mpiganaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa akipigana pambano la pili chini ya kocha mpya, Virgil Hunter akijaribu kurejesha hadhi yake kwenye ndondi baada ya kupigwa mfululizo na Lamont Peterson na Danny Garcia.
Khan, mshindi wa Medali ya Fedha katika Olimpiki ya mwaka 2004 mjini Athens, Ugiriki ushindi wake umetokana na mafundisho mazuri ya kocha wake mpya, Hunter huko San Francisco.
Amir Khan akishangilia ushindi wake
Mawindo: Amir Khan akijiandaa kutupa konde
Chini: Diaz akiwa amemuangusha Khan raundi ya nne, lakini Muingereza huyo aliinuka na kuendelea na pambano hadi kushinda. Chini anahesabiwa.
Ua...: Khan akijiandaa kumchapa Diaz
Mpambano ulikuwa mkali...
Kitu cha uhakika: Khan akipiga ngumi ya kutokea chini