Baada ya story ya mwanadada Jacqueline wolper kutolewa nje pamoja na vitu vyake kuzagaa kwenye vyombo vya habari hususani magazeti, tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili tupate ukweli wa jambo hilo na kuamua kumtafuta hewani
Mwandishi: Mambo Jack, mzima wewe? Jacqueline Wolper: Mi mzima, vipi salama?
Mwandishi: Salama kabisa, vipi kuhusu hii habari ya kutolewa vitu nje ya nyumba? Nini tena kimetokea?
Jacqueline Wolper: Hiyo habari sio ya ukweli kama ilivyo, ukweli ni kwamba sijatolewa vitu ila nimehama sehemu niliyokuwa nakaa na kuhamia sehemu nyingine
Mwandishi: Kitu gani kilitokea mpaka kukawa na hizi habari za kutolewa vitu nje? Na ulikuwa unakaa wapi?
Jacqueline Wolper: Mwanzo nilikuwa nakaa ,Mbezi beach, kwenye apartment ya kama USD 1500 kwa mwezi, na nilikuwa nakaa mwenyewe, na kama unavyojua huwa nawalea wadogo zangu na muda huo walikuwa wapo chuo. Ila walipomaliza nikaona badala ya mimi kukaa mwenyewe ni bora nitafute nyumba nyingine mbili ili wakae wenyewe na mimi nikae mwenyewe.
Ndo maana nikahama huko mbezi beach. Sa sijui hao wanaosema nimetolewa vitu nje wanatoa wapi hayo maneno. Labda kama walipiga picha wakati nahama na kuamua kujitengenezea stori.
Mwandishi: Unahisi ni kwanini wameandika kuwa umetolewa vitu nje?
Jacqueline Wolper: Mmmh! Siwezi kujua na wala hainisadii, maana sio kweli. Mi sukuona sababu ya kulipa hizo hela kwa mwezi wakati naweza kukaa kwenye nyumba nzuri ya $800 au mia $900 kwa mwezi na nikawatafutia wadogo wangu nyumba nao wakae kwa gharama hiyo hiyo na kwa uhuru wao.
Kwangu mimi haina maana hata kidogo kwa sasa kulipa hela zote bila sababu, Wakati nipo mwenyewe ilikuwa sawa ila sasa it doesn’t make sense at all. Kuna mambo mengine ya muhimu ya kufanya. Na isitoshe suala la foleni. So sijui waliondika hivyo wanatafuta nini kwangu.
Mwandishi: Basi tunashukuru sana Jack kwa maelezo yako.
Jacqueline Wolper: Asanteni sana
JUU ni baadhi ya Picha za nyumba anayoishi jackline wolper sasa baada ya kuhama mbezi