Wednesday, 1 May 2013

HAYA AVRIL AFUNGUKA!! CHEKI ANASEMAJE HAPA


Leo ikiwa ni birthday ya mtoto mzuri 'Hakuna Yule' hit maker wa Ogopa Djs ya Kenya Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril, ametua jijini dar es salaam jana na sababu ya ujio wake ni vitu vikubwa viwili.

Akihojiwa katika kipindi cha XXL kupitia Clouds fm Avril amesema ujio wake hapa bongo kwanza ni ku-celebrate birthday yake na fans wa Tanzania, na pili ni ku-launch single yake mpya aliomshirikisha Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yuko ziarani barani Ulaya, party ilifanyika usiku wa kuamkia jana (April 30) pale Elements club.

Kuhusiana na maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu ya tetesi za kuwepo kwa mahusiano baina yake na Diamond Platnumz ambaye alimshirikisha Avril katika video ya Kesho, Avril amekana kuwepo kwa uhusiano wowote zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida na wa kikazi. "Hakuna kitu chochote kati yangu na diamond we are just friends na relationship yetu ni proffesional relationship katika muziki", alisema Avril.

Kama ulikuwa hujui hii ndio birthday party ya kwanza kwa Avril kufanya, birthdays zake zote zilizopita alikua anasheherekea kwa kuchill tu nyumbani na familia yake.

Leo Avril ametimiza miaka 26,alizaliwa April 30, 1986 huko Nakuru Kenya.

we wish you a happy birthday Avril na karibu sana Tanzania