Wednesday, 8 May 2013

DILI LA MOURINHO KUTUA CHELSEA LABUMA, SASA NJIA NYEUPE KWAKE KUTUA MAN UNITED

DILI la Jose Mourinho kurejea Chelsea linaweza kushindikana na hivyo kufungua milango ya yeye kwenda kurtihi mikoba ya Sir Alex Ferguson Manchester United.

Habari hizo ni dalili tosha kwake kuwa nafasi ya kutua Old Trafford, baada ya Sir Alex Ferguson kuamua leo kustaafu kufuatia kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 27.
 
Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich hayuko tayari kuilipa Real Madrid fedha za kuvunja mkataba, licha ya kumalizana na Mourinho awali juu ya maslahi yake binafsi.
 
Waiting in the shadows: But Jose Mourinho's return to Chelsea could be off over a compensation row
Waiting in the shadows: But Jose Mourinho's return to Chelsea could be off over a compensation row
 
Snag: Roman Abramovich is unhappy at paying the compensation fee needed to free Mourinho's contract
Ameshituka: Roman Abramovich hafurahii kulipa kulipa ada ya mkataba wa Mourinho Real
 
Abramovich alimlipa Mourinho na timu yake nzima ya benchi la ufundi Pauni Milioni 18 alipomfukuza mwaka 2007 na ili kuvunja mkataba wake na Madrid inaaminika zitatakiwa kulipwa Pauni Milioni 20 za msimu mmoja.
 
Mreno huyo bado ni mtu anayepewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Rafa Benitez Stamford Bridge, lakini Chelsea inataka mamlaka zaidi katika kusajili wachezaji zaidi ya iliyokuwa nayo wakati anawasili akitokea Porto mwaka 2004.
 
Kwa muda mrefu Mourinho amekuwa akitabiriwa kuwa mrtihi wa Ferguson, lakini kocha wa Everton, David Moyes sasa ndiye anapewa nafasi kubwa kutwaa mikoba hiyo.
 
Benitez alisema jana kwamba dunia nzima inajua Mourinho yuko njiani kurejea Stamford Bridge.
 
Alisema: "Unajua kwamba mwakani kocha mwingine atakuwa hapa  — hiyo iko wazi sana. Kila mtu anajua nani atakuwa hapa. Nitaelekeza fikra zangu katika kazi yangu.
 
"Unafikiri kweli atahitaji ushauri wangu (juu ya kazi)? Sifikiri hivyo,"alisema.
 
Calling time: Sir Alex Ferguson has ended his 27-year reign at Manchester United
Wakati wa kuondoka: Sir Alex Ferguson amehitimisha miaka yake 27 kazini Manchester United
 
Return: Mourinho won back-to-back Premier League titles with Chelsea in 2005 and 2006
Anarejea: Mourinho alishinda mfululizo ubingwa wa Ligi Kuu England akiwa na Chelsea mwaka 2005 na 2006