
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati
 ya Maandalizi ya Mazishi ya Albert Mangweha tunapenda kuwaatarifu rasmi
 kuwa mwili wa marehemu Ndugu yetu, mpendwa wetu Albert Mangweha 
utawasili [leo] tarehe 04/06/2013 saa nane mchana na ndege ya Shirika la
 Ndege la Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu 
Nyerere (Terminal One).
Tunaomba mjitokeze kwa wingi kwa ajili ya kumpokea ndugu yetu, mpendwa wetu Albert Mangweha.
Taarifa hii kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mapokezi na Mazishi. Asanteni na Mungu awabariki.