
Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .
  Akizungumza
 ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema 
kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo 
imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu 
upelelezi.
Kamanda Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.
  Hali
 kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi 
wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya 
kuomboleza ..
  Hata
 hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo wamekaidi agizo 
hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA ,
 hali iliyoleta  mvutano kati ya
 viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao baada ya kukaidi amri ya jeshi hilo mabomu yalirindima uwanjani hapo.
  
    Baadhi
 ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje...