Mwigizaji anayekubalika zaidi nchini na aliyeshinda tuzo ya 
mwigizaji bora wa kiume 2012/2013 kupitia tuzo za steps entertainment 
zilizofanyika siku ya tarehe 15/06/2013 jijini Dar es Salaam, Jacob 
Steven maarufu Zaidi kama JB ama “Bonge la bwana” amechaguliwa kuwa 
balozi wa shiriki lisilo la kiserikali la Oxfam International linalojihushisha na mambo mbalimbali ya kuondoa umasikini duniani kupitia kampeni yake ya grow kwa upande wa Tanzania.
Usimikaji huo ulioambata na utoaji wa tuzo maalumu kwa watu washindi hao sita wakiwemo Dina Marious
 wa clouds FM, Mheshimiwa Halima Mdee (Mbunge wa kawe), Mheshimiwa 
Shy-Rose Bhanji (Mbunge), Mchoraji katuni maarufu Masoud Ally wa 
Kipanya, Mbunifu wa mitindo Tanzania Khadija Mwanamboka na Blogger 
maarufu nchini Shamimu Mwasha.
GROW ni kampeni ya kimataifa inayoendeshwa na shirika la Oxfam. 
Kampeni hii inataka tuoteshe na kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa 
chakula, uimarishaji wa haki na mustakabali wa wanawake wazalishaji wa 
chakula na pia kulinda mandhari ya uoto na uhalisia wa sayari yetu.
Dunia inazalisha chakula cha kutosha lakini watu wapatao milioni
 moja wanalala bila kula kila siku. Mbaya zaidi, idadi kubwa ya hao ni 
wanawake wazalishaji na watoto. 
