BAADA ya kukamilisha uhamisho wake kutua 
Barcelona, Neymar ambaye anaungana na Lionel Messi kuunda safu mpya kali
 ya ushambuliaji, ameweka wazi malengo yake.
Mbrazil huyo alisafiri moja kwa moja 
kwenda Hispania baada ya Brazil kutoa sare ya 2-2 nyumbani na England 
mjini Rio de Janeiro Jumapili, na katika mahojiano aliyofanyiwa kwenye 
Uwanja wa Nou Camp alisema: "Nipo kumsaidia na kumsaidia Messi kuendelea
 kuwa mchezaji bora duniani,".
Neymar alipokewa kifalme katika Uwanja wa 
Ndege wa Barcelona - kabla ya kupelekwa kwenye ofisi za klabu hiyo kwa 
ajili ya kupigwa picha akiwa na jezi ya Blaugrana kisha kwenda kufanyiwa
 vipimo vya afya.

Neymar alitambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Barcelona Nou Camp jana

Mbrazil huyo amesaini Mkataba wa miaka mitano Catalan

Neymar akionyesha uwezo wake wa kuchezea mpira mbele ya umati wa Nou Camp


Neymar anaungana na 'mchawi' huyu Lionel Messi kuunda safu kali ya ushambuliaji Barcelona

Rais wa Barcelona, Sandro Rosell akimkaribisha Neymar Nou Camp

Neymar akipungia mkono mashabiki Nou Camp 

Neymar akisalimiana na mashabiki watoto wa Barca Uwabnja wa Nou Camp

Neymar akifanyiwa vipimo vya afya
