KIUNGO Marouane Fellaini anataka kujiunga
na katika orodha ya wachezaji wanaolipwa Pauni 100,000 kwa wiki Arsenal,
lakini The Gunners tayari imetenga dau kubwa kwa usajili mwingine.
Huku mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo
Higuain akiwa njiani kutua kwa dau la Pauni Milioni 22, The Gunners
wataelekeza nguvu zao katika kuboresha safu ya kiungo.
Tayari kuondoka: Marouane Fellaini anataka kujiunga na Arsenal
Fellaini ametokea kuwa mshindani mkuu wa
nafasi mbele ya zoezi la Arsene Wenger kusaka kiungo, lakini dau kubwa
linalotakiwa linaleta kama uhamisho huo utafanikiwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25,
ambaye kwa sasa analipwa Pauni 75,000 kwa wiki Everton, anataka kukuza
kiwango chake cha sasa mshahara.
Kutoka kikosi cha sasa cha Arsenal, ni
Theo Walcott na Lukas Podolski peke yao wapo katika kiwango cha mshahara
cha Pauni 100,000 kwa wiki.
Mbali na kudai mshahara mkubwa, Arsenal
pia watalazimika kufika bei anayouzwa Fellaini, Pauni Milioni 22- ambayo
itafanya dili zima la usajili wake liendee kwenye Pauni Milioni 50.
Injini: Fellaini anaweza kuboresha safu ya kiungo ya Arsenal
Mtu muhimu: Kocha mpya wa Everton, Roberto Martinez anakabiliwa na changamoto ya kumbakiza Fellaini
Na wakati Wakuu wa Arsenal wanataka huduma
ya Fellaini majira haya ya joto, inafahamika kwamba watalazimika kufika
bei inayotakiwa.
Zaidi ya hapo, Fellaini anataka uhakika wa
kucheza katika safu kuu ya kiungo Uwanja wa Emirates. David Moyes
alikuwa anamtumia kama mshambuliaji wa pili Everton.
Zenit St Petersburg, ambayo ina fedha za
kumwaga, kiasi cha kuweza kufika bei ya Mbelgiji huyo, itatoa upinzani
kwa The Gunners katika kuwania saini ya Fellaini.
Manchester City pia imeonyesha nia ya kumsajili Fellaini, lakini ilipunguza kasi tangu Yaya Toure asaini kuongeza Mkataba.