KITUO cha Redio cha Napoli, Marte 
kimetangaza kwamba dau la Pauni Milioni 49.3 limetolewa na Chelsea kwa 
ajili ya mshambuliaji  Edinson Cavani.
Katika taarifa ya jana usiku, Radio Marte 
ilitangaza: "Tumepokea taarifa kutoka ofisini kwa vyanzo vya kuaminika 
kwamba, Napoli imekubaliana dili la kuiuzia Chelsea Cavani.

Kitu moto: Chelsea sasa ipo katika nafasi ya kumnasa Edinson Cavani
"Rafa Benitez pia amebariki, lakini kabla 
ya kutangaza rasmi, Napoli inataka kupata mshambuliaji atakayeziba pengo
 la Il Matador.
"Aurelio De Laurentiis", klabu itasomba kiasi cha Euro Milioni 58, sawa na dili la Ezequiel Lavezzi kwenda PSG mwaka jana.
"Mchezaji huyo atajiingizia mshahara wa Euro Milioni 8.5 kwa msimu pamoja na haki za picha,". Habari zimevuja kama kwamba Cavani
 ametangaza anataka kukutana uso kwa uso na Rais, Aurelio de Laurentiis 
na kuna taarifa kwamba Manchester United nayo imo kwenye mbio hizo. 
Mshambuliaji huyo wa Uruguayna baba yake 
awali walionyesha nia ya kutaka kwenda Real Madrid. Klabu hiyo ya 
Hispani iliwasiliana na Napoli, lakini sasa itabidi waipiku ofa 
iliyotolewa na Chelsea.

Anayetakiwa sana: Man United na PSG pia zinamtaka Cavani