NYASI za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo zinatarajiwa kuwaka moto kwa mpambano wa watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga. Huo utakuwa mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wakiwa tayari wamewavua ubingwa wapinzani wao wa jadi, Simba SC. BIN ZUBEIRY inaendelea kukuletea mfululizo wa makala za kuelekea pambano hilo linalobeba picha halisi ya soka ya Tanzania na leo tunafanya tathmini ya vikosi vyote, hususan wachezaji wanaotarajiwa kuchezeshwa jioni hii Taifa. Endelea.
Simba SC |
WATU wansema kikosi cha Simba kinaundwa na wachezaji wenye umri mdogo, wasio na uzoefu waliopandishwa kutoka kikosi cha vijana na kwa sababu hiyo, Yanga yenye kikosi kizima cha wachezaji wazoefu inapewa nafasi ya kushinda leo.
Lakini ukirejea kikosi cha kwanza cha Simba, unagundua huo si kweli- bali katika kikosi cha Simba kuna damu change kadhaa zilizoonyesha uwezo mkubwa kiasi cha kuaminiwa, hadi baadhi ya wachezaji ‘mafaza’ wakawekwa kando kama akina Haruna Moshi ‘Boban’, Juma Nyosso, Amir Maftah na wengineo.
Ni wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao wameudhihirisha katika mechi za Ligi Kuu walizocheza, kiasi cha wengine kuitwa hadi timu ya taifa, Taifa Stars katika kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Morocco Juni 8 ugenini kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani kama Haruna Chanongo.
Kikosi cha Simba ambacho kimekuwa kikicheza siku za karibuni ni; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Mussa Mudde, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto au Abdallah Seseme, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amri Kiemba na Chanongo.
Wakati mwingine, William Lucian ‘Gallas’, Hassan Hatibu, Rashid Ismail, Edward Christopher chukua nafasi katika kikosi cha kwanza, ingawa leo kuna uwezekano ‘mtu mzima’ Felix Sunzu akaanza.
Kwa Yanga, ukuta unajulikana, Ally Mustafa ‘Barthez’ atakuwa analindwa na Mbuyu Twite kulia, kushoto Oscar Joshua, katikati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan, wakati kiungo mkabaji atakuwa mtu mzima, Athumani Iddi ‘Chuji’.
Mbele, kulia atakuwa anateleza Simon Msuva, kushoto Haruna Niyonzima katikati Frank Domayo na washambuliaji wanaweza kuanza Didier Kavumbangu na Hamisi Kiiza. Tutazame maeneo au wachezaji ambao wanatarajiwa kuwa kivutio leo.
Kocha Mfaransa wa Simba SC, Patrick Liewig |
LANGONI…
Akianza Juma Kaseja, au Abbel Dhaira kwa upande wa Simba SC, yeyote bado lango la Wekundu wa Msimbazi litakuwa kwenye mikono salama. Kwa uzoefu wake wa mechi za watani, hadi sasa akiwa amecheza mechi 26 tangu mwaka 2003, Kaseja anapewa nafasi kubwa ya kuanza leo mbele ya Uganda One, Dhaira.

Upande wa Yanga SC, Barthez ataanza na hiyo itakuwa mechi yake ya kwanza akiwa Jangwani kudaka dhidi ya Simba na ya pili kwa ujumla katika mapambano ya watani, pamoja na ile aliyodaka akiwa Simba dhidi ya Yanga Aprili 19, mwaka 2009 timu hizo zikitoka 2-2.
Yanga SC |
SAFU ZA ULINZI:
Kwa Simba Chollo bila shaka atacheza kulia, kushoto Miraj Adam na katikati Mudde na Kapombe, wakati kiungo wao mkabaji atakuwa Jonas Mkude. Ukiondoa Miraj, wengine wote waliobaki wana uzoefu wa mapambano ya watani na kwa ujumla tayari ni wazoefu. Huyu dogo Miraj pamoja na kwamba atakuwa akicheza dhidi ya Yanga kwa mara ya kwanza, lakini tarajia mambo mazuri kutoka kwake. Kijana anajua soka akikaba vizuri na kusaidia mashambulizi pia. Hasumbuliwi na watu wenye miili mikubwa, yeye anahangaika na mpira na huwa hachezi rafu. Huu ni ukuta wenye sifa za kuitwa ukuta bora.

Kwa Yanga, Twite hapana shaka ataanza kulia, lakini kushoto anaweza kuwa Oscar Joshua au David Luhende, wakati katikati watakuwa Cannavaro na Yondan nyuma ya kiungo wao mkabaji, Chuji. Uzuri wa Twite zaidi ni katika kusaidia mashambulizi na kurusha mipira kama anapiga, ila kwenye ukabaji anapokutana na wachezaji wenye kasi na uwezo wa kumiliki mpira aina ya Messi, Ngassa na Chanongo huwa uchochoro. Oscar hatabiriki, lakini Luhende hakuna shaka atakaba vema na kusaidia mashambulizi pia.
Miraj Adam kulia atakuwa na shughuli na Simon Msuva leo |
SAFU YA KIUNGO:
Kwa Simba SC, Mkude atacheza chini, mbele yake Seseme au Kazimoto, pembeni Ngassa na Chanongo. Mkude tayari mzoefu wa mechi za watani na hakuna shaka ataiunganisha timu vizuri tu pale chini. Tofauti ya Seseme na Kazimoto ni uzoefu tu, lakini kwa uwezo wa kuichezesha timu wote wazuri. Watu wa pembeni, Ngassa na Chanongo wote wana kasi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kupia chenga na kukimbiza, kupangua ngome. Wote wanaweza kufunga ingawa uzoefu unamfanya Ngassa awe zaidi ya Chanongo. Ni matarajio Simba leo itashambulia zaidi kutokea pembeni. Mabeki wa Yanga watakuwa na kazi.

Upande wa Yanga SC, Chuji atacheza chini, juu yake Domayo, kulia Msuva na kushoto Niyonzima. Hakuna shaka juu ya Chuji pale chini na zaidi zile pasi zake ndefu kwa watu wa pembeni huzalisha mashambulizi vizuri sana. Domayo ni starehe tu kwa wana Yanga pale mbele na pembeni nako Msuva wengi sasa wanaijua kasi yake, wakati Niyonzima japo hana kasi ya kulinganisha na wenzake, lakini ni mtu anayefanya vitu vya uhakika. Msuva na Niyonzima, wana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kupangua ngome, kupiga chenga na kufunga. Dhahiri mabeki wa Simba watashughulishwa leo.
Kiemba kulia na Niyonzima |
SAFU YA USHAMBULIAJI:
Kwa Simba Simba SC bado haijulikani haswa patakuwaje mbele, ingawa Amri Kiemba atakuwa mmojawapo. Anaweza kuanza Messi au Sunzu? Haijulikani. Ila kama tayari unaye uwanjani Ngassa na Chanongo vema kumfanya Messi mchezaji wa akiba na kama Sunzu ataanza atasaidia kuongeza kashikashi kwenye safu ya ulinzi ya Yanga SC. Kiemba ni fundi ambaye amedhihirisha ubora wake kwa mara nyingine na anatarajiwa kabisa kung’ara leo.

Kwa Yanga, wawili kati ya watatu hawa Said Bahanuzi, Didier Kavumbangu na Hamisi Kiiza ndiyo wataanza. Kuna uwezekano mkubwa Bahanuzi akaingia kipindi cha pili akitokea benchi na kama Kiiza ataanza na Kavumbangu Yanga itakuwa na safu kali ya ushambuliaji.
Ngassa kulia na Kavumbangu kushoto |
KIKUBWA SOKA:
Pamoja na ubora wa wachezaji, lakini mifumo na falsafa za uchezaji zitachangia sana matokeo katika mchezo wa leo. Tumejionea katika mechi za msimu huu, timu zote zinaweka mpira chini, mpira unapitishwa kwenye njia zake mabao yanatafutwa kwa utengenezaji wa nafasi. Tumekwishatoka kwenye Simba na Yanga za enzi zile, ‘hakuna kuremba’ na sasa soka inachezwa. Tunasubiri kuona makocha, Mfaransa wa Simba SC, Patrick Liewig na Mholanzi wa Yanga SC, Ernie Brandts wametuandalia nini siku ya leo.

Asante mdau wa soka mahmoud Zubeiry kwa picha na habari