WARENO Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho walitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati Atletico Madrid inaifunga Real Madrid katika muda wa nyongeza Uwanja wa Bernabeu usiku wa jana kuwapiku wapinzani wao wa Jiji ndani ya miaka 14 na kubeba Kombe la Mfalme, Copa del Rey.
Bao la Miranda dakika ya 99 ndilo lililoipa ushindi Atletico. Bao la kichwa la Ronaldo liliipa Madrid bao la kuongoza dakika ya 14, lakini Diego Costa akasawazisha dakika 10 kabla ya mapumziko.

Bao la ushindi: Joao Miranda akifunga bao la ushindi na kuipa Atletico taji la Copa Del Rey

Mwali: Gabi akiinua taji la Copa Del Rey


Majanga: Mesut Ozil akiwa mwenye masikitiko baada ya kumaliza msimu bila taji

Kadi nyekundu: Cristiano Ronaldo alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kwa kumpiga Gabi

panda jukwaani: Refa Clos Gomez akimtoa nje Jose Mourinho

Undava: Luka Modric (kushoto) akionyeshana ubabe na Koke dakika za mwishoni

Bao la kwanza: Cristiano Ronaldo akifunga bao lake

La kusawazisha: Diego Costa akimtungua Diego Lopez kuisawazishia Atletico

Walipowasili: Basi la Real Madrid likiwasili uwanjani kwa ajili ya mchezo

Mashabiki waAtletico Madrid

Kocha wa Atletico, Diego Simeone akishangilia bao la ushindi

Masikini Jose Mourinho amemaliza msimu bila taji

Michael Essien na Filipe Luis