Patcho Mwamba na Steven Kanumba katika moja ya filamu.
MWIGIZAJI na mwanamuziki wa Dansi Patcho Mwamba anasema kuwa kuna  wakati ambao anatokewa na marehemu Kanumba akiwa amelala na kumwita huku  akimsihi kutema mema na kuwa na upendo katika jamii maana anaamini kuwa  Duniani maovu yamezidi na kitu kikubwa ni wasanii hawapendani, chuki,  wivu vimetawala kwao.
Patcho Mwamba mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
Patcho Mwamba katika pozi.
Patcho Mwamba msanii wa filamu.“Kama mtu umeishi naye vizuri inakuwa si rahisi kumsahau kwa mara  moja hasa kama anakuwa mtu muhimu kama rafiki yangu marehemu Kanumba  mara nyingi ananitokea ndotoni na kuniita kunisihi kutenda mambo mema  kwa watu nisiwe na roho mbaya nipende watu kama yeye alivyokuwa anapenda  watu na kuwa kipenzi cha watu,”anasema Patcho.
Patcho Mwamba ni mwigizaji ambaye anakubalika na watayarishaji wengi  kwa sasa baada ya kuvumbuliwa na marehemu Kanumba na kumpa filamu yake  ya kwanza kuigiza ya This is it na kumshirikisha karibu filamu nyingi  alizokuwa akiigiza marehemu, filamu alizoigiza Patcho ni This is it,  Uncle JJ, Love and Power, Young Billionaire , More than pain na filamu  nyingine nyingi. 
