BAO la Ben Watson katika dakika ya mwisho kabisa jioni hii limeipa Wigan ubingwa wa Kombe la FA kwa mara ya kwanza kabisa ikiichapa Manchester City 1-0 kwenye Uwanja wa Wembley.
Nyota huyo aliyetokea benchi alifunga kwa kichwa akiunganisha kona na kuwa shujaa wa mashabiki wa Wigan na kumfanya Roberto Mancini arejee nyumbani mikono mitupu.
Man City ilimaliza pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Zabaleta kutolewa nje kwa kadi nyekundu daika ya 84.
Katika mchezo huo, kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Silva, Toure , Barry/Dzeko dk90, Nasri/Milner dk54, Aguero na Tevez/Rodwell dk69.
Wigan: Robles, Boyce, Scharner, Alcaraz, Espinoza, McCarthy, McArthur, Gomez/Watson dk81, McManaman, Kone na Maloney.
Rahaaa: Ben Watson akishangilia bao lake la ubingwa wa FA
Joe Hart akiruka bila mafanikio
Mancini sasa anaweza kutimuliwa Manchester City akimpisha kocha wa Malaga, Manuel Pelligrini
Sergio Aguero akijutia kupoteza nafasi ya kufunga
Kiungo wa City, Yaya Toure akikabiliana na Paul Scharner wa Wigan
Refa mudaa: makocha wote walikuwa bize jana
Dua iliyopokewa: Wachezaji wa Wigan wakiomba dua kabla ya mechi
Shabiki wa Manchester City akifurahia na Kombe bandia kabla ya mechi
Mashabiki wawili wa Manchester City wakiwa wamevaa sura bandia za Mancini jana Wembley
Kombe halisi: Kombe la FA likiwasilishwa uwanjani