KLABU ya Galatasaray ina mpango wa kumsajili beki wa John Terry kwa mkataba wa miaka mitatu, ikimpa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki.
Klabu hiyo ya Uturuki inayotumia fedha nyingi katika usajili, ambayo iliwasajili Didier Drogba na Wesley Sneijder Januari, inaamini inaweza kumshawishi Nahodha huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 32 kumaliza mapenzi yake na Stamford Bridge baada ya miaka 14 ya mafanikio.
Anakwenda Uturuki? Beki wa Chelsea, John Terry (kulia) anatakiwa na Galatasaray
Terry kwa sasa mbele ya kocha wa muda, Rafa Benitez si mchezaji wa uhakika katika kikosi cha kwanza Chelsea, jambo ambalo linahatarisha nafasi yake hata mbele ya kkcha ajaye.
Nahodha huyo wa zamani wa England, ambaye amekuwa akiwekwa benchi Benitez, amebakiza zaidi ya mwaka mmoja katika mkataba wake ambao analipwa Pauni 150,000 kwa wiki.
Wataungana: Terry anaweza kuungana na na Didier Drogba ambaye sasa anachezea mabingwa hao wa Uturuki