VINARA Barcelona watalazimika kusubiri kwa wiki nyingine kushangilia taji la La Liga baada ya Cristiano Ronaldo kufunga mabao mawili katika ushindi wa Real Madrid inayoshika nafasi ya pili wa mabao 4-3 wakitokea nyuma dhidi ya Real Valladolid jana.
Kama Real isingeshinda, ushindi wa Barca dhidi ya Real Betis Uwanja wa Nou Camp Jumapili ungewahakikishia taji la nne ndani ya miaka mitano, wakiwa kileleni kwa pointi 13 zaidi zikiwa zimebaki mechi nne zenye wastani wa pointi 12.
Valladolid, ambayo haijachukua pointi Bernabeu kwa zaidi ya muongo, ilipata bao la kuongoza dakika ya nane wakati Oscar Gonzalez alipomtungua kipa wa Real, Diego Lopez.
Mvunjaji rekodi: Cristiano Ronaldo amefunga mabao mawili na kufikisha mabao 199 Real Madrid
Nguvu: Ronaldo akienda hewani kuipiga kichwa cha nguvu kumtungua kipa wa Valladolid
WAFUNGAJI BORA LA LIGA
44 Lionel Messi (Barcelona)
33 Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
26 Radamel Falcao (Atletico Madrid)
19 Alvaro Negredo (Sevilla)
Roberto Soldado (Valencia)
16 Ruben Castro (Real Betis)
15 Piti (Rayo Vallecano)
Real ilisawazisha dakika ya 26 wakati Marc Valiente alipobabatiza shiti la Angel Di Maria na kujifunga, kabla ya Ronaldo kufunga bao lake la kwanza jana kwa kichwa dakika sita baadaye.
Valladolid ilifunga kupitia kwa Javi Guerra dakika ya 35 na Kaka akaisawazishia tena Real dakika nne baadaye.
Ronaldo alifunga tena dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika akiunganishwa kwa kichwa kona, hilo likiwa nao la 33 kwa Mreno huyo katika msimu huu wa ligi.
Maumivu: Ronaldo kuna wakati aliumia jana