
Mwakilishi
  wa Tanzania Fedha Kessy akiwasalimu  mashabiki wake kwa kuwapungia  
bendera ya Tanzania. Kulia ni mtangazaji wa Shindano la Big Brother The 
 Chase 2013 Ik.

Kundi
 la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini likitoa burudani wakati wa 
uzinduzi wa show ya Big Brother-The Chase iliyorushwa Live na Channel za
 DStv 197 na 198 jijini Johannesburg usiku huu. Shindano la Big 
Brother-The Chase limedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchin mbalimbali za Afrika kushuhudia Live uzinduzi huo.

Mwakilishi
 kutoka Tanzania Nando akihojiwa na Mtangazaji wa  kipindi hicho Ik 
wakati wa uzinduzi wa show hiyo.Kushoto patna wa Nando Mshiriki kutoka 
Namibia Cleo.

Mtangazaji
 IK akifanya mahojiano na Patna wa Mwakilishi wa Tanzania Mshiriki 
kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa Shindano la Big Brother The 
Chase lililozinduliwa rasmi leo jijini Johannesburg Afrika Kusini ambapo
 washiriki watakaa ndani ya jumba hilo kwa siku 90 na mshindi 
kujinyakulia kitita cha Usd 300,000. Kulia ni Fedha Kessy mshiriki 
kutoka Tanzania.

Mtangazaji
 IK akimtambulisha rasmi mshiriki kutoka Tanzania Fedha Kessy kwa Patna 
wake Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa shindano hilo 
leo jijini Johannesburg.

Baadhi
 ya waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliopata 
mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa shindano hilo Live kutoka Kampuni ya 
Multichoice Africa. Wa pili kulia ni Operations Manager wa Mo Blog 
Zainul Mzige aliyeiwakilisha Tanzania.

Kutoka
 kushoto ni Mwandishi wa habari kutoka Afrika Kusini  Munya, Buhle na 
Thato kutoka Ofisi za Multichoice Afrika Kusini wakishow love back stage
 wakati wa uzinduzi wa shindano la Big Brother The Chase.

Wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali mbele ya camera yetu.

Mini Bar iliyondaliwa maalum kwa wageni waalikwa.

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Kenya Stella Mwangi a.k.a STL akitoa burudani huku akipewa sapoti na Manager wake.

(Picha na Dewji Blog)