UWANJA maarufu wa Brazil, Maracana Stadium umefunguliwa tena jana usiku baada ya miaka mitatu ya ukarabati, na upo tayari kwa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 na sherehe za ufunguzi za Olimpiki ya mwaka 2016.
Mchezo wa kwanza kufanyika kwenye Uwanja huo baada ya kukamilika kwa ukarabati wake uliikutanihsa timu ya Marafiki wa wa Ronaldo dhidi ya Marafiki wa Bebeto jana.
Rais wa Brazil, Dilma Rousseff, rais wa zamani, Luiz Inacio Lula da Silva na watu wengine wenye majina makubwa waliokuwa miongoni mwa watu 30,000 waliohudhuria ufunguzi huo.
Washington, mshambuliaji wa zamani wa Fluminense, alifunga bao la kwanza jana kwa kichwa dakika ya 16, wakati Ronaldo, ambaye enzi zake anacheza hakuwa kufunga kabisa kwenye Uwanja huo, jana alifunga bao lingine.
Maracana ulikuwa mmoja wa viwanja vikubwa duniani, wakati watu 200,000 waliposhuhudia Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1950 kati ya Brazil na Uruguay. Pia ni uwanja ambao, Pele alifunga bao lake la 1,000 mwaka1969.
'Sinagogi la Soka': Ukarabati umekamilika Uwanja wa Maracana uliopo Rio de Janeiro, Brazil na umefunguliwa jana kwa magwiji wa soka Brazil, wakiongozwa na Ronaldo na Bebeto kucheza baina yao.
Heshima: Welder Antonio Pereira aliungana na gwiji wa Brazil, Ronaldo katika sherehe za ufunguzi
Bao la kwanza: Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Washington alifunga bao la kwanza jana katika Maracana mpya
Busu la uepndo: Washington akibusu nyasi za Uwanja huo
Mamia kadhaa walikandia zoezi hilo kwa njia ya amani, wakibeba mabango ya kubeza kwamba Serikali ya nchi hiyo itapata hasara katika uwekezaji wake huo
Timbwili: Polisi wakiwakamata watu waliokuwa wakifanya vurugu nje ya Uwanja wa Maracana Ijumaa
Welder Antonio Pereira alipewa heshima ya kwenda kumpasia mpira Ronaldo kuanzisha mchezo huo wa sherehe za ufunguzi.
Ronaldo, ambaye aliiwezesha Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1994 na 2002, pia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Fainali zijazo za Kombe la Dunia
Gwiji: Mshindi wa fainali mbili za Kombe la Dunia, Ronaldo akiupungia umati jana. Enzi zake anacheza soka hakuwaghi kufunga bao Uwanja wa Maracana
Bado anaweza: Ronaldo, aliyeifungia Brazil mabao 62 katika mechi 98, akipokea pasi jana
Anakumbushia: Ronaldo akipasua...
Mkongwe: Bebeto, ambaye alikuwa Nahodha wa timu nyingine, akimtoka mchezaji jana
Anakwenda na mpira: Mkongwe wa Brazil, Junior, ambaye aliichezea Brazil mechi 70, akiambaa na mpira jana
VIDEO: Ronaldo akifunga Maracana