Mh.Balozi  Ramadhan Mwinyi ndiyo alikuwa mgeni mharikwa katika sherehe hizo za  maadhimisho ya miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar  zilizofanyika jijini New York. Sherehe hiyo ilihudhiliwa na watanzania  wengi kutoka katika miji ya jilani na New York kama New Jersey,  Delaware, Massachusetts na Connecticut. Watanzania waliungana kwa pamoja  kwa kula chakula na kucheza music sambamba na vinywaji baridi.
Katibu wa jumuiya ya watanzania New York bwana Shaban Mseba akisoma risala katika sherehe hizo za muungano
Mwenyekiti  wa jumuiya Hajji Khamis akiongea machache mbele ya watanzania  waliojitokaza katika sherehe hizo zilizofanyika New York katika  kitongoji cha New Rochelle.
Dr  Chemponda alikuwa nae kama anavyoonekana katika picha akiongea machache  juu ya jinsi gani anavyo ujua muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mama  Ashura Duale nae anaujua sana muungano wa Tanganyika na Zanzibar na  alikuwa mmoja ya washuhuda wa uchanganyaji mchanga wa pande zote mbili  za Tanganyika na Zanzibar
Hii ndiyo cake ya muungano ikiwa mezani
Ukodak  wa pamoja katia ya Dr Chemponda, kushoto mama Ashura katikati, na  kushoto kwa mama Ashura ni mama mwenye nyumba wa Mh. Balozi Mwinyi, Na  kulia na Mh. Balozi Mwinyi
Ukodak mbele ya cake 
Mh. Balozi akikata Cake tayari kwa kuwalisha wana muungano walio jitokeza katika sherehe hizo
Mh.  Balozi Ramadhani Mwinyi akimrisha kipande cha cake mama mwenye nyumba  wake kabla ya watu wengine awajapata nafasi hiyo. Kwa picha zaidi ya  sherehe hizo zilizofanyika katika jiji la New york bofya read more.
 
 



 
 
 
 
 
 
