Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, 
Godbless Lema wakiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu 
(Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Freeman Mbowe na Godbless Lema wakiwa katika Uwanja wa Soweto jana 
mchana wakati zoezi la kuchukua vipimo mbalimbali likiendelea chini ya 
usimamizi wa wataalamu toka jeshini.
Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako 
kwa kitu ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo
 zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo 
tanki hilo lilishambuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari hii 
ya matangazo lina majeraha mawili mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu
 chenye ncha ambacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.
Dereva wa mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bwana Benny akiwa hospitali.
James Ole Millya na Mbunge Lema wakimjulia hali mmoja wa majeruhi walilazwa hospitali ya Seliani.