
WASANII
 wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’  na 
Jacqueline Wolper Massawe ‘Wolper’ wamemaliza bifu lao lililokuwa  
likifukuta kama moto wa kifuu mwishoni mwa wiki mbili zilizopita.
Akizungumza
 na mwandishi  wetu katikati ya wiki hii, Baby alisema  alikuwa Mkoani 
Geita kwa ziara ya kikazi lakini alipigiwa simu na Wolper  akimuomba 
msamaha kutokana na tofauti zao zilizosababishwa na nyumba ya  kupanga. 
“Nimeona
 bora yaishe kwa sababu Wolper amekubali kosa na  mimi siwezi kuendeleza
 bifu lakini kama asingeniomba msamaha  tungefikishana mbali,’’ alisema 
Baby Madaha na kuongeza:

“Nimemalizana
 na Wolper ila kesi itabaki kwa mwenye nyumba,  nitapambana naye hadi 
atakaporejesha mkwanja wangu japokuwa nimepata  nyumba nyingine maeneo 
ya Mikocheni.”
Wolper
 na Madaha waliingia  kwenye bifu zito baada ya Madaha kukuta nyumba 
aliyoilipia shilingi  milioni 3.6 kama kodi maeneo ya Kinondoni jijini 
Dar imechukuliwa na  Wolper  kabla yeye hajahamia.