Kisiki; Kevin Yondan na wenzake wanakula kipupwe Protea hivi sasa |
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA SC wameweka kambi katika hoteli ya Protea, Oysterbay, Dar es Salaam leo wakitokea Pemba walipokuwa kwa wiki nzima kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
YANGA SC wameweka kambi katika hoteli ya Protea, Oysterbay, Dar es Salaam leo wakitokea Pemba walipokuwa kwa wiki nzima kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga watalala hapo wakiweka akili zao sawa tayari kwenda kujaribu kulipa kisasi cha kupigwa 5-0 na Simba SC katika mechi ya kufunga msimu uliopita Dar es Salaam.
Mapema jana, kocha Mkuu wa Yanga SC, Ernie Brandts alisema anaamini kikosi chake ni bora na ana kila sababu ya kuwafunga wapinzani wake wa jadi, Simba SC kesho.
Akizungumza akiwa Pemba, ambako timu yake imeweka kambi tangu Ijumaa ikijifua vikali kwa ajili ya mchezo huo, Brandts alisema kwamba matumaini ya ushindi Jumamosi ni makubwa kutokana na ubora wa kikosi chake.
“Nina timu bora, wachezaji bora, uwezo wa wachezaji wangu ni wa hali ya juu, mshikamano na umoja katika kikosi ni wa hali ya juu, morali na mtazamo wa kila mchezaji ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo, kwa hiyo nina kila sababu ya kujivunia kikosi changu kuibuka na ushindi,” alisema Brandts.
Akiwazungumzia wapinzani wake, beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, alisema Simba wana timu nzuri, lakini hiyo haimpi presha kwani kikosi cha Yanga kimekamilika kila idara.
“Nina timu bora. Nia, uwezo na sababu ya kushinda mchezo huo tunayo, hivyo wana Yanga wakae mkao wa kushangilia ushindi na ubingwa siku ya Jumamosi,”alisema.
Kwa upande wake, Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri, wachezaji wana morali ya hali ya juu lengo lao ni kuhakikisha wanashinda mchezo wa Jumamosi na kuwapa furaha wana Yanga.
Kuelekea mchezo huo, Yanga tayari imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu kutokana na pointi zake 57, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Azam FC imejihakikishia nafasi ya pili kwa pointi zake 52 na inaweza kumaliza ligi na pointi 55 ikishinda mechi yake ya mwisho dhidi ya JKT Oljoro keshokutwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na Simba waliokuwa mabingwa watetezi, watakuwa wa tatu kwa matokeo yoyote keshokutwa.
Kikosi cha Yanga kilichoweka kambi Samail Hotel, mkabala na beki ya PBZ, kimekuwa kikifanya mazoezi kwenye wa Uwanja wa nyasi bandia wa Gombani.