Tuesday, 14 May 2013

WALIONASWA WAKIFANYA MAPENZI NA MBWA NI WANAFUNZI WA CHUO KIKUU..... UONGOZI UMEWAKANA

 

CHUO Kikuu cha Kiufundi cha Mombasa (TUM) kimekanusha madai kwamba wanafunzi wake ni makahaba wanaofanya vitendo vya ngono na mbwa.
 
Kwenye barua ya kukana dai hilo iliyopelekwa kwenye vyombo vya habari baada ya chuo hicho kutajwa kama chenye wanafunzi 11 waliokamatwa Nyali juzi kwa kashfa ya ngono, chuo hicho kilisema kina mikakati mikali ya kufundisha maadili.

“Tunapenda kusahihisha uongo na kusema ukweli juu ya suala linaloendelea kugonga vichwa vya habari juu ya ngono
za kinyama na mbwa,” ilisema barua hiyo.


Barua hiyo iliyotiwa sahihi na Naibu Mkuu wa chuo hicho Prof Josphat Mwatelah ilisema, “Tungependa kuweka wazi kwa wazazi wote na umma kwamba madai ya watu (wasichana) waliokamatwa wiki jana huko Nyali Mombasa kwa masuala ya ukahaba na kufanya mapenzi na mbwa kuwa ni wetu ni uongo. Wasichana hao si wanafunzi wetu wala hawahusiani kivyovyote na chuo chetu."

Barua hiyo iliendelea kwamba pekuapekua za stakabadhi za chuo hicho kikuu hazikuonyesha hata jina moja kwamba ni la mwanafunzi wao.
 
“Kikosi cha walinda usalama wetu pamoja na wachunguzi maafisa wa polisi vimethibitisha kwamba watu hao kamwe si wanafunzi wetu”, ilisisitiza barua hiyo.


Nakala hiyo iliendelea, “Chuo chetu kina kitengo madhubuti cha kuelekeza wanafunzi na kuwatia nia na maadili mema ya kijamii. Chuo chetu pia kina kitengo madhubuti cha kuongoza wanafunzi juu ya maovu yanayokithiri nchini Kenya,” ilisema.

Barua ilieleza kwamba TUM imejitolea kuendeleza mafunzo bora kwa wanafunzi wake ili hatimaye wawe wananchi wenye maadili, tabia na mienendomizuri katika jamii.
 
“Tunavionya  vyombo vya habari kwa kutaja jina la chuo chetu kuhusiana na kashfa hii na kwa kuharibu jina na sifa ya chuo chetu pasipo kuthibitisha taarifa yenyewe kwanza na kutaka vituombe msamaha kupitia umma”, iliongeza barua hiyo.

Suala hiyo limezua mjadala mkali na kushutumiwa nchini na nchi za ng’ambo huku mashirika ya dini na ya umma yakitaka uchunguzi kamili na wageni wanaohusika kwenye njama hiyo wakamatwe, washtakiwe kasha warudishwe makwao hatimaye.
 
Polisi hapo Jumapili walidokeza kwamba wanamtafuta mwanamke mmoja kutoka Karatina anayetuhumiwa kuzama kwenye lindi la biashara hiyo haramu na ambaye ameingia gizani tangu wasichana hao 11 kukamatwa huko Nyali.