Tuesday, 14 May 2013

TAKUKURU MKOA WA NJOMBE YAPELEKA WATUMISHI 16 WA SERIKALI MAHAKAMANI

  Mkurugenzi wa TAKUKURU Dr. Edward Hosea

Jumla ya Watu 16 Mkoani Njombe Wamefikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Rushwa Huku Wengi Wao Wakiwa ni Watumishi wa Serikali Katika Wilaya za Njombe,Makete na Ludewa.

Miongoni Mwa Watu Hao ni Pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji Pamoja na Wakuu Katika Idara Mbalimbali Kwenye Halmashauri Hizo za Wilaya.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoani Njombe Charles Nakembetwa Amesema Matokeo ya Kufikishwa Mahakamani Kwa Watendaji na Watu Hao ni Mafanikio Dhidi ya Mapambano ya Rushwa Mkoani Njombe na Kusema Kuwa Wataendelea Kuwafuatilia Wale
Wote Wanaojihusisha na Vitendo Hivyo.

Kamanda Nakembetwa amesema Makundi Mbalimbali katika Jamii tayari yameshapatiwa Elimu wakiwemo Askari Polisi na Magereza

Sanjari na Elimu hiyo Lakini pia ameeleza kuwa TAKUKURU Mkoa wa Njombe imefanikiwa kufungua KLABU za Wapinga Rushwa katika Shule zote za Mkoa wa Njombe.

Pamoja na Mambo mengine Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe amesema kwa kawaida Mtumishi wa Serikali anapobainika na Makosa kama Hayo TAKUKURU Hutoa taarifa kwa Mwajiri Wake.

Aidha TAKUKURU Mkoani Njombe Imewataka Wananchi Kutoogopa Kutoa Taarifa Juu ya Vitendo Vyovyote Vinavyoashiria Rushwa Kwenye Maeneo Yao.
 
Na Gabriel Kilamlya