Friday, 3 May 2013

Sintah amficha mpenzi wake; Kisa!! awahofia warembo wa bongo movies…! Fuatilia Zaidi hapa…


Habari tulizozipata kutoka kwa mdau mmoja (Jina Kapuni) wa karibu sana na Christine John maarufu kama “sintah” zinasema kuwa mwandada huyo maarufu hapa nchini anaogopa kumuweka wazi mpenzi wake amabye insemekana ni raia wa kigeni (mzungu) kwa madai kuwa anaogopa sana baadhi ya tabia za wasanii wa bongo movies kuibiana wanaume pindi wajuapo ni mpenzi wa fulani.

Rafiki wake huyo alisema kuwa, kwa mujibu wa Sintah, jamaa huyo amemsahaulisha matatizo ya mapenzi kwani hana wivu kama wanaume wa kibongo na sio muongo wa mapenzi.

Sintah ambaye pia ni blogger maarufu nchini na mtangazaji maarufu wa kipindi cha harusini na sintah, amesisitiza kuwa kamwe hatakaa amuweke wazi kipenzi chake huyo na kusema kuwa wanaosubiri ili waje kumpora waendelee kusubiri sana kwani kamwe hawataweza kuharibu uhusiano wake huo.