Watanzania tunafuraha kubwa kwa sababu wapiganaji wa Jeshi letu la Wananchi Tanzania (JWTZ) wamewasili mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani wakiwa salama.
Wiki iliyopita, Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete alikabidhi Bendera kwa Kiongozi wa Bataliani ya wapiganaji wa JWTZ wanaokwenda nchini humo, kwenye hafla iliyofanyika Msangani Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Siku moja kabla ya kufika kwa kikosi cha pili cha Tanzania (cha kwanza kilienda kimya kimya) waasi wa M23 waliendesha kampeni kubwa sana ya kuhamasisha wananchi wa GOMA waandamane kupinga ujio wa askari wa Tanzania mjini GOMA.
Kiongozi wa siasa wa M23 akiongea na wakazi wa Kibumba na huku hutuba yake ikirushwa na redio inayomilikiwa na waasi na kusikika mjini GOMA ,aliwaasa wakazi wa GOMA wafanye maandamano makubwa siku vikosi vya TANZANIA vitakapowasili.
CHAKUCHEKESHA ni kwamba, tofauti na waaasi walivyo tegemea , hakuna Mtu hata mmoja aliye andamana! Hii inaonyesha wazi kuwa waasi hawa wameshapoteza ushawishi walio kuwa nao hapo awali.
PROPAGANDA ZA UONGO WA M23
Waasi wa M23 wamekuwa wakiendesha vita ya kisaikolojia ya kuvichonganisha vikosi vya UN na wakazi wa jimbo la Kivu wenye asili ya kitusi.
M23 wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara na kusambaza vipeperushi kuwa WATANZANIA wamekuja kumsaidia KABILA kuwateketeza WATUSI (maauaji ya halaiki) kitu ambacho si kweli.
TUJIULIZE..!!! ..Kuna watusi wangapi wanaoishi Tanzania? si tungeanza na hao kama ndio lengo letu! ...Hayo ni maneno ya mfa maji..!!!
Timu ya utangulizi ya ICGLR ambayo ripoti yake ndo ilitumika na AU na baadaye baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha azimio la kupeleka BRIGEDI yakuingilia kati mzozo wa Kongo ilikuwa na makamanda kutoka majeshi yote ya nchi za maziwa makuu zikiwemo nchi za Rwanda, Uganda, Congo, Burundi nk:
Makamanda hao walienda mjini Goma mwezi wa tisa mwaka jana wakiongozwa na Brigedia jenerali James Mwakibolwa .Sasa kama lengo letu ni kuteketeza watusi , je, Rwanda ingekubali kweli?....Hayo ni maneno ya mfa maji..!!!
Hata mazoezi ya awali ya kupambana na vikundi hatarishi kwenye nchi za ukanda wa Africa mashariki yalifanyika RWANDA chini ya jina la The Command Post Exercise (CPX).
Mazoezi hayo yaliongozwa na Brigedia jenerali James Mwakibolwa akisaidiana na Brig. Gen Jacques Musemakweri wa Rwanda. Hili la kuangamiza watusi ni kuweweseka kwa M23.
TUMESHAVUA NGUO, NI LAZIMA TUOGE..!!
Watanzania wengi ni watu wa kulaumu, wengi wanasubiri baya litokee kwa askari wetu huko DRC basi waanze kulaumu.
Ni Vyema serikali ikaanza kutuandaa watanzania kwa kuendesha semina kwa waandishi wa habari kuhusu uzalendo wa nchi yetu.
Mfano mzuri ni MALAWI, wao kwa sasa kwenye mzozo wa ziwa nyasa waandishi wote na taifa kwa ujumla bila kuzingatia vyama vyao wala dini wako kwenye "state of union".
Nachukulia mfano mwandishi wa makala wa gazeti la nyasa times ( Malawi Nyasa Times - Malawi breaking news in Malawi ), Patricia Masingaambaye kwenye makala yake ya tarehe 5 mwezi huu amewafananisha viongozi wa Tanzania na Adolf hitler!.
Patricia anadai Tanzania ni wapenda vita na ndo maana tunag'ng'ania ziwa malawai (ziwa nyasa) ...Mwandishi huyo ameandika kuwa tunag'ang'ania kwenda CONGO kwa ajili ya mali iliyoko CONGO na tunang'ng'ania ziwa malawi kwa kuwa chini yake yamegundulika mafuta na gesi!.
Patricia Masinga pia anadai watanzania hatujui kiingereza ndio maana tumeng'ng'ania tunaushahidi wa uongo.
Naye mhariri wa NYASA TIMES katika kile alicho kiita TAHARIRI MAALUM ya tarehe 28/2/2013 alidai kuwa kama TANZANIA tunataka nusu ya ziwa nyasa basi turudi kwenye win - win situation, yaani turudishe ardhi yote iliyokuwa chini ya utawala wa MARAVI KINGDOM ambayo ilitawala eneo kubwa la kusini mwa Tanzania kabla ya kuja wakoloni .
Haya ni matusi makubwa kwetu na juhudi za wenzetu kuzitetea nchi zao .Nadhani hii ni chachu tosha kwa waandishi wa habari wa Tanzania.
Tuuvue UCHAMA na badala yake tuuvae UZALENDO ili Tuilinde Tanzania ya Kesho..!!