WAKATI Sir Alex Ferguson anaachia ngazi,  mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney ameomba kuondoka pia Old  Trafford wakati ambao habari zinasema klabu iko mbioni kumrejesha  Cristiano Ronaldo.
Saa kadhaa baada ya Ferguson kuthibitisha  atastaafu ukocha United mwishoni mwa msimu, akimpisha kocha wa Everton,  David Moyes, inabainika Rooney alimuambia Ferguson wiki mbili zilizopita  anataka kuanza maisha mapya.
Wakati huo huo, inagundulika, Mtendaji  Mkuu wa United, David Gill alikuwa mjini Madrid kukutana na Jorge  Mendes, wakala maarufu Mreno anayemuwakilisha Ronaldo. 
Vyanzo vimesema  jana usiku kwamba, United inajiamini itamrejesha mchezaji huyo  iliyemuuza Real Madrid kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 80,  mwaka 2009. 

Jinsi walivyokuwa: Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo wakati wanacheza pamoja Manchester United

Katika bluu: Chelsea ina matumaini ya  kumnasa mshambuliaji huyo wa England kwa Pauni Milioni 25 ahamie  Stamford Bridge msimu ujao