Mratibu wa Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMAISP), Ofisi ya Makamu wa Rais, ndugu Joseph Kihaule (kushoto) akikabidhi sehemu ya vitabu hivyo kwa Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Misitu na Uhifadhi ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Prof. Yonika M. Nganga.
Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kupitia Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA-ISP) imekabidhi vitabu vinavyohusiana na Taarifa za Hali ya Mazingira na Mkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Vyuo Vikuu mbalimbali hapa nchini.
Vitabu hivi ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira katika kujenga uwezo kwa wadau kuweza kuelewa na kutunza mazingira. Ofisi kwa kupitia programu hii itaendelea kushiriana na wadau mbalimbali kuelimisha umma dhana zima ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira hapa nchini.(Picha na Michuzi)
Mratibu wa Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMAISP), Ofisi ya Makamu wa Rais, ndugu Joseph Kihaule (kushoto) akikabidhi baadhi ya vitabu kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Idrisa Kikula (katikati), kulia ni Prof. Kinabo akishuhudia.
Mratibu wa Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMAISP), Ofisi ya Makamu wa Rais, ndugu Joseph Kihaule (kulia) akikabidhi baadhi ya vitabu kwa Naibu Mrajisi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijini cha Dodoma, Prof. Innocent J.E Zilihona.
Hapa akikabidhi baadhi ya vitabu hivyo kwa Kaimu Makamu Mkuu wa Mafunzo, ndugu Edwin Lyanda wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Iringa. Aidha vitabu vingine vilikabidhiwa kwa Vyuo Vikuu vya St. John’s, Dodoma, Chuo Kikuu cha Kiislamu, Morogoro na Chuo Kikuu cha St. Augustine Tawi la Morogoro (Jordan University)