Monday, 6 May 2013

NAIBU Waziri wa Fedha Janeth Mbene ametoa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Shilingi Mlioni 7 kwa timu 16 za Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya.

 Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Senyamule alisema lengo la michuano hiyo ni kuleta Umoja kwa vijana wa Wilaya ya Momba ikiwa ni pamoja na kukuza vipaji ili kupata Wachezaji wa Timu ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla kutokana na Mji wa Tunduma kutoa Wachezaji wengi wazuri.

NAIBU Waziri wa Fedha Janeth Mbene ametoa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Shilingi Mlioni 7 kwa timu 16 za Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya.

Timu zikiingia uwanjani
Mkuu wa wilaya ileje na viongozi wengine wakipokea timu zikiingia uwanjani  
 Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Senyamule akisalimiana na wachezachi

 
NAIBU Waziri wa Fedha Janeth Mbene ametoa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Shilingi Mlioni 7 kwa timu 16 za Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya.
  
Vifaa  hivyo ni pamoja na jezi za mpira wa miguu jozi 16 ambazo zilizawiwa kwa timu zote zilizoshiriki Michuano ya Ligi ya Mpira wa Miguu iliyofanyika katika Mji Mdogo wa Tunduma iliyojulikana  kwa jina la CCM Super Cup.

Mbali na vifaa hivyo vya michezo Naibu Waziri alitoa pia kitita cha Fedha Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya washindi watatu wa Mwanzo ambapo Mshindi wa Kwanza alijinyakulia Shilingi Laki tano(500,000/=), Mshindi wa pili Shilingi Laki tatu(300,000/=) na mshindi wa tatu alijinyakulia Shilingi Laki mbili(200,000/=).

Timu zilizoibuka kidedea katika michuano hiyo ni pamoja na Timu ya Nasele Fc  ambayo ilikuwa mshindi  wa Kwanza na mshindi wa Pili ikiwa ni Timu ya Super Rangers zote za Mpemba huku Mshindi wa Tatu ikichukuliwa na Timu ya Eagle Fc  kutoka katika Mji mdogo wa Tunduma.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Fedha, Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Senyamule alisema lengo la michuano hiyo ni kuleta Umoja kwa vijana wa Wilaya ya Momba ikiwa ni pamoja na kukuza vipaji ili kupata Wachezaji wa Timu ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla kutokana na Mji wa Tunduma kutoa Wachezaji wengi wazuri.

Alisema katika Michuano hiyo ilipata mafanikio makubwa kutokana  na kukusanya watu wengi bila kujali itikadi za Vyama vya Siasa  ambapo pia aliwaomba wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kudhamini michezo ili kuinua viwango na kutoa ajira kwa vijana.
  
Aidha kabla ya kuwa mgeni rasmi katika Fainali ya Michuano hiyoiliyokamilika Mwishoni mwa Wiki iliyopita Mkuu huyo wa Wilaya alipata fursa ya kutembelea vikundi mbali mbali vya uzalishaji mali na Wafanyabiashara wa Tunduma.

Senyamule aliwaahidi wafanyabiashara na wajasiliamali hao kuwasaidia kutoa elimu ya ujasiliamali ili kukuza vipato vyao kutokana nay eye kuanzisha mpango wa kutoa elimu kwa wajasiliamali Wilayani Ileje ambao wameonekana kunufaika na mpango huo.
 

 PICHA NA Mbeya yetu