Thursday, 2 May 2013

MWENYEKITI WA CHADEMA ATAKA SHERIA YA KUNYONGA MAJANGILI ILI KUNUSURU UTAJIRI WA NCHI YETU

 mwenyekiti wa chadewa mheshimiwa Mbowe akiongea mjengoni

Sakata la Biashara haramu ya meno ya Tembo inayoendelea kushamiri nchini limechukua sura mpya baada ya Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni FREEMAN MBOWE kuliomba Bunge kutunga sheria itakayohalalisha mtu atakayekutwa na nyara za Serikali kinyume na taratibu kunyongwa.

Akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii Mjini Dodoma MBOWE amesema, licha ya tafiti kuonesha kwamba, ikiwa hali ya ujangili haitadhibitiwa ndani ya kipindi cha miaka saba ijayo idadi ya tembo waliopo Tanzania itatoweka.

Kwa upande wake Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chadema Mchungaji PETER MSINGWA ameitaka Serikali kuachana na mtindo wa kubeza inapopewa taarifa za kiuhalifu na badala yake ichukue hatua na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote wanaohusika.

Hali hiyo pia inaonesha kumkera Mbunge wa Muhambwe kupitia NCCR –Mageuzi FELIX MKOSAMALI ambaye anahoji uhalali wa Serikali kuendelea kuwepo madarakani kwa madai ya kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi wa rasilimali zilizopo nchini.

Akitoa majumuisho ya hoja hizo za Wabunge, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii LAZARO NYALANDU amesema, Serikali itayafanyika kazi maoni ya Wabunge hao ili kudhibiti vitendo vya ujangili kwa lengo la kuwalinda wanyamapori nchini.