Tuesday, 7 May 2013

MUSWADA WA KUZUIA MAANDAMANO NCHINI WAANDALIWA


Katika hali ya kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi aliliambia bunge jana  jioni  kwamba serikali  imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Waziri Nchimbi alisema kuwa  hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa....


Alisema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.

Huenda  azimio hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.


Ikumbukwe ni hapo juzi  tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali  wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kudhibiti wapinzani kuiimarisha CCM.


Credit: JF