Saturday, 4 May 2013

Mourinho kuwabakiza Lampard na Terry Chelsea, Falcao na Alonso kukomaza kikosi cha Chelsea

image
Kocha wa Real Mdrid ambaye amevumishwa kuwa karibu kujiunga na Chelsea Jose Mourinho ameazimia kuhakikisha anawabakiza wachezaji wakongwe wa klabu hiyo John Terry na Frank Lampard.

Wachezaji hao wawili ambao ni manahodha wa Cheslea wamekuwa na wakati mgumu chini ya kocha wa Muda Rafael Benitez ambaye amekuwa hawatumii kwenye mechi nyingi huku akiamini kuwa umri wao mkubwa unamaanisha kuwa hawawezi kupata nafasi kama walivyokuwa na umri mdogo.

Frank Lampard anakaribia kumaliza mkataba wake ndani ya Chelsea na uongozi wa klabu hiyo umegoma kumuongezea mkataba jambo ambalo mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakilipinga vikali. Hata hivyo Mourinho ambaye anawaamini sana wachezaji hao amemuagiza mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich kuhakikisha Terry na Lampard wanabaki Chelsea kwani wako kwenye mipango yake .

Zaidi ya hapo Mourinho pia anadaiwa kukanusha usajili wa Radamel Falcao ambaye kwa muda mrefu amekuwa kwenye mipango ya usajili wa Chelsea pamoja na Xabi Alonso ambaye amehusishwa na usajili wa Chelsea endapo Mourinho atarudi.