Friday, 3 May 2013

MOURINHO KOCHA MPYA CHELSEA KWA MSHAHARA MNONO, AMALIZANA NA ABRAMOVICH LONDON

KOCHA Jose Mourinho amekubali dili la kujiunga tena na Chelsea na atarajea rasmi Stamford Bridge Julai 1, kwa mujibu wa taarifa jana usiku.
 
Kocha huyo wa Real Madrid inadaiwa kupata chakula cha jioni na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich katika mgahawa wa La Famiglia Magharibi mwa London ambako inasemekana amekubali ofa ya mshahara wa Pauni Milioni 10 kwa mwaka – ingawa bado kunahitajika mjadala wa kuruhusiwa kuondoka Real. 
 
Abramovich atatakiwa kuilipa Real Pauni Milioni 12 kama gharama za kumng'oa kocha huyo machachari duniani.
 
Heading to Chelsea? Jose Mourinho looks likely to leave Real Madrid at the end of the season
Anakwenda Chelsea? Jose Mourinho anaonekana kama ataondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu
 
Chelsea itatangaza dili hilo kabla ya kwenda kwenye ziara yao ya kujiandaa na msmu mpya, Mashariki ya Mbali, ambayo inamaanisha kwamba mechi ya kwanza ya kurejea kwa Mourinho itakuwa ya kirafiki dhidi ya Singha All Stars XI nchini Thailand Julai 17.
 
Msaidizi wa zamani wa Mourinho, Andre Villas-Boas, Alhamisi alisema anafikiri dili hilo la kumrejesha bosi wake wa zamani katika klabu hiyo aliyopata nayo mafanikio limefanikiwa. 
 
Kocha huyo anayeinoa Spurs kwa sasa, ambaye alifanya chini ya Mourinho katika klabu za Porto, Chelsea na Inter Milan, alisema hawezi kuzungumza na swahiba wake huyo juu ya kuondoka Madrid na kurejea Ligi Kuu England hadi atamke rasmi kurejea kwake.
 
"NIna uhakika kiasi cha kutosha uamuzi umekwishachukuliwa,"alisema Mreno mwenzake huyo.
"Inasemekana kwamba anafurahi kurejea England na Chelsea ni moja ya klabu zinazosaka kocha inaonekana sana, kwa kiasi kikubwa sana atatua huko. 
 
Giving the thumbs up: Roman Abramovich has reportedly agreed a deal to bring Mourinhio back to Stamford Bridge
Amekubali: Roman Abramovich ameripotiwa kukubali dili la kumrejesha Mourinhio Stamford Bridge
 
Where the deal was done: Italian restaurant La Famiglia in Chelsea
Sehemu ambako dili lilifanyika: Mgahawa wa Kitaliano wa La Famiglia in Chelsea
 
The glory years: Mourinho helped Chelsea win the Premier League
Miaka ya mafanikio: Mourinho aliisaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu

Wakati huo huo, taarifa Hispania zinasema kwamba Mourinho anajaribu kumnasa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski ili kuipiku Bayern Munich atue naye Chelsea ikiwa atarajea.
 
Promising: Andre Villas-Boas has done an excellent job at Tottenham
Anakuja vizuri: Andre Villas-Boas amefanya kazi nzuri Tottenham
 
Support: Chelsea's fans make no secret of their desire to see Mourinho return Sapoti: Mashabiki wa Chelsea hawafichi mapenzi yao Mourinho 
 
In 2004: Villas-Boas was part of Mourinho's backroom staff when he first arrived at Chelsea
Mwaka 2004: Villas-Boas alikuwa mmoja wa wasaidizi wa Mourinho alipowasili mara ya kwanza Chelsea