Tuesday, 14 May 2013

Mmmh! Wema Sepetu aanikwa na Diamond, aeleza na sababu za kumrekodi! Hii sasa imepitiliza!


Baada ya kimya kirefu sana, hatimaye msanii Diamond Platnumz amefanya interview na Mwanadada Sporah Njau na kuamua kueleza ya "chumbani zaidi" kuhusu mrembo mwenye mvuto sana wa bongo movies, Wema Sepetu na kueleza sababu za yeye kuamua kumrekodi sauti na kuiweka clip hiyo wazi kwenye vyombo vya habari. Msikilize Diamond hapa kwa kubofya haya maneno yenye rangi umsikie akifunguka ya moyoni. 

Katika mengi aliyoyazungumza Diamond, alsema kuwa amevumilia mengi sana kwa mrembo huyu ila ilifika mahali akaaona kuwa imetosha na hawezi kuendelea tena kwa madai kuwa Wema hakuwa mwaminifu kwake.

Akizungumzia suala la kumrekodi alisema kuwa ameamua kuafanya hivyo kutokana na usumbufu alikuwa akiupata toka kwa mwanadada huyu mpaka kutishia penzi lake na mwanadada Penny, hivyo alirekodi clip hiyo kwa ajili ya Penny ili kuonesha kuwa sio yeye anayemtaka Wema bali wema ndo anamsumbua ila kwa bahati mbaya clip hiyo itaenda kwenye vyombo vya habari.

Juhudi za kumpigia simu wema hazikuweza kupatikana kwani simu yake iliita bila kupokelewa ila bado tunajaribu kufanya mawasiliano naye ili tusikie maoni yake kuhusu maneno haya ya Diamond

Tupe maoni yako!