Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu kulipuka kitu kinachosadikika kuwa ni bomu katika kanisa moja jijini Arusha
Matiro amesema kufuatia tukio hilo lililotokea Arusha hakuna budi wananchi kuwa makini kwa kuwa kumekuwa na muingiliano wa watu ambao wanafika kwenye wilaya yake na wengi wao wakiwa wageni lakini hawatoi taarifa na pia hakuna mtu mwingine ambaye anatoa taarifa kuwa kuna watu wageni ambao hawafaamiki na wameingia kwenye eneo hilo
Amesema si lazima watu ama mtu huyo afike kwako lakini endapo ataonekana hata kwa jirani ni lazima utoe taarifa ili ahojiwe na kujulikana ametoka wapi
“zamani kulikuwa na utaratibu mzuri ambao hivi sasa tutaurejesha, watu walikuwa hawakubali kumpokea mtu yeyote mgeni bila taarifa zake kujulikana wazi ikiwemo kwa viongozi, lakini hivi sasa hicho kitu hakipo” alisema Matiro
Katika hatua nyingine mkuu huyo amewataka wale wote wenye kanda ama CD zenye uchochezi wa kidini kuzisalimisha kwenye vyombo vya usalama kwa kuwa ni kosa kisheria na atakayekamatwa nazo atachukuliwa hatua za kisheria
Amesema cd hizo zinachochea uvunjifu wa amani na zitaweza kupelekea vita ya kidini ambyo ni vita hatari kuliko zote, hivyo kuwataka wenye nazo kuzipeleka wenyewe kwenye vyombo vya usalama na kusisitika kila mtu kulilinda amani iliyopo wilayani mwake isivunjike