Monday, 13 May 2013

MFANYABIASHARA ALIYEFUMANIWA NA MWANAFUNZI GESTI APIGWA FAINI YA 640,000

 
YULE mfanyabiashara  wa jijini Dar ambaye hivi karibuni alifumaniwa gesti akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili, huenda akapandishwa kizimbani siku yoyote.....

Kwa mujibu wa dada wa mwanafunzi huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe , baada ya mfanyabiashara huyo kufumaniwa na binti huyo mwenye umri wa miaka 16, aliahidi kutoa fedha za Kimarekani dola 400 (zaidi ya Sh. 640,000) kama faini kwa kitendo hicho.

Hata hivyo, pamoja na kukubali kutoa kiasi hicho, mfanyabishara huyo hakutimiza ahadi yake na kuamua kuingia mitini.
 
Dada wa mwanafunzi huyo amedai  kuwa   mfanyabiashara huyo anasakwa ili wamburuze mahakamani kutokana na mwisho wa mwezi uliopita kushindwa kutimiza ahadi yake.
 
“Aliandika kwa mkono wake kwamba atamlipa huyu mwanafunzi fedha hizo kama fidia ili akalipie ada ya kuendelea na masomo, lakini mpaka leo hii hajaonekana na wala simu yake ya mkononi haipatikani, tukimkamata tutamburuza mahakamani kwa sababu sheria hapa Bongo hazifuatwi kabisa kwani tulitarajia vyombo husika vingeingilia kati lakini hakuna lolote,” alisema dada huyo.

Aidha, dada huyo alisema kuwa wanatarajia kwenda kuchukua hati ya kumkamata mfanyabiashara huyo ‘RB’ katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ili waweze kumsaka.

“Ushahidi tunao tena wa uhakika kabisa, kaandika kwenye karatasi na katia saini yake, tena mwandishi naomba na zile picha alizopigwa akiwa chumbani na mdogo wangu ili zinisaidie katika ushahidi wa mahakamani,” alisema dada huyo huku akionesha karatasi ambayo waliingia makubaliano ya kulipwa dola hizo 400 na mfanyabiashara huyo.

Jumatano ya Aprili 24, mwaka huu mfanyabiashara huyo alifumaniwa na denti huyo katika chumba namba 107 ndani ya gesti moja iliyopo Kinondoni, Dar