Na Bryceson Mathias
MEYA wa Halmashauri ya Musoma na Katibu wa Madiwani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Alex Kasurura (pichani), ameelezea wasi wasi wake asivyokuwa na Imani na uadilifu wa baadhi ya vinara na waelekezi uundaji Katiba unaoendelea sasa nchini.
Wasiwasi wa Kasurura unakuja kukiwa na Malalamiko kila Kona ya nchi wasivyoridhishwa na Mchakato Mzima wa Uchaguzi wa wajumbe wa Mabarza hayo katika Mitaa, Vijiji, Kata na Wilaya, kwamba uligubikwa na Hila, Rushwa, Undugu na Itikadi za Vyama na kuathiri zoezi hilo.
Akizungumza na Wandishi Dodoma wiki hii akiwa Njiani kuelekea Arusha, Kasurura alisema, wapo watu waliojikita Kileleni kuelekeza na kuchambua Maoni ya wananchi kuhusu katiba hiyo lakini hawana Uadilifu. Iwapo walikosa uadilifu kwa watu wa kawaida makwao, wataweza ya Taifa?
“Kuna viongozi miongoni mwa kamati hiyo, wasifu na uadilifu wao (back ground) kwa siku za nyuma una mashaka, maana waliwatendea vibaya hata mmoja wa watoto kwao, atashindwaji kulitendea ubaya Taifa lisilomjua?alisema Kasurura bila kuwataja kwa majina yao.
Alisema wao wanaowajua wanafahamu hata Kiini cha Mchakato wa kudai Katiba, kimsingi ulianzishwa na Wanaharakati, Wabunge na Wapenda Amani kuhakikisha Wananchi wanapata Haki na Stahili za Utu wao uliofinyangwa na kudumazwa na Wakoloni.
Kama wabunge ndio wanaojua Ulegevu, Udhaifu na Mapungufu ya Serikali yao, wao kama wawakilshi, ndio wenye nafasi nzuri (Position) zaidi, kutoa maoni wakilenga udhaifu na ulegevu wanaoufahamu! Sasa kama tunataka Jamii itoe mchango wao bila kuisimamia, tunataka Katiba iliyokufa!
Aidha alisema, Sababu za Uhitaji wa Katiba ulioshinikizwa pia na Vyama vya Upinzani, ni pamoja na Kero za Muungano, Mamlaka ya Rais, Tume Huru ya Uchaguzi, na Mambo mengi yanayowanyima Haki wananchi, hivyo walio na nafasi nzuri kuhoji na kuchambua ni Wabungeambao wanajua shida na papungufu ya watu wao na Serikali.