Sunday, 5 May 2013

MACHINGA WALIOPEWA JEURI NA MBUNGE MSIGWA KUVUNJA SHERIA WAKWAMA IRINGA CHEKI HAPA KINACHOENDELEA HUKO





Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa ambae ni kaimu mkuu  wa  mkoa wa Iringa Dr Leticia  Warioba  akitembelea maeneo hayo  kuona jinsi ambavyo  polisi  walivyojipanga  kupambana na  wavunjaji  wa sheria Machinga

 Askari  wa  FFU  mkoani  Iringa  wakiweka  ulinzi mkali  eneo la Mashine  tatu  ambalo si eneo  rasmi la biashara  ila mbunge  wa  jimbo  la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) aliwataka  machinga hao  kuvunja sheria na  kulitumia eneo hilo la barabara kwa  biashara
Ulinzi mkali kweli  kweli  eneo la Mashine  tatu Miyomboni mjini Iringa  hivi  sasa ,Machinga  wakubali yaishe  wasitisha  kuvunja  sheria
Machinga  waliotaka kufanya  biashara  eneo hilo wakiamua kuondoa eneo hilo la Mashine  tatu  baada ya  polisi  kukesha  wakilinda  eneo hilo usiku  kucha  leo

NGUVU  ya umma waliopewa wafanyabiashara  ndogo ndogo (Machinga ) na mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji  Peter  Msigwa (Chadema) kuvunja  sheria kwa  kufanyabiashara maeneo ambayo hayaruhusiwi  imeshindwa baada ya jeshi la polisi kutumia mbinu mpya na ya kiusalama  zaidi  kuthibiti nguvu ya umma.

Hatua  ya  jeshi la  polisi  kubuni  mbinu  hiyo ya  kuthibiti  nguvu ya umma inayovunja sheria  imekuja baada ya  wiki  iliyopita machinga  hao  kujigamba kwa  kufanyabiashara  eneo  hilo la mashine  tatu  kwa kumsikiliza mbunge  wao msigwa  badala ya sheria

Askari  hao  wa kikosi  cha  kutuliza ghasia  (FFU) mkoa  wa Iringa  wakiwa wamejiimarisha  zaidi  usiku  wa kuamkia  leo  wamekesha  katika  eneo  hilo la Mashine  tatu  pamoja na mkuu  wa  wilaya ya Iringa Dr Leticia  Warioba hatua iliyopelekea   machinga kushindwa  kuvunja  sheria .

Mtandao  huu umeshuhudia ulinzi mkali kweli kweli  eneo  hilo  huku magari  zaidi ya 7 ya  polisi ,Karandinga la  polisi na askari  zaidi ya 50  wakizunguka  mji  huo wa  Iringa  kama njia ya  kuthibiti mbinu  zisizokubarika za uvunjaji  wa  sheria.


Wakizungumzia  hatua ya  jeshi  la  polisi  mkoa wa Iringa  kutumia nguvu  nyingi  zaidi  katika  kuthibitia uvunjaji  huo  wa  sheria  baadhi ya  wananchi  wa  mji  wa Iringa  walipongeza hatua  hiyo kwa madai  kuwa  bila nguvu ya  ziada ya  polisi suala la  wanasiasa  kutafuta umaarufu kwa  kuruhusu  sheria  ivunjwe  ungeendelea  na ungesababisha madhara  makubwa  zaidi.

Alisema mfanyabiashara   Anna Sanga  kuwa mbali ya mbunge  Msigwa  kuonyesha  kuwatetea  machinga  ila njia inayotumika sio kwani  ni njia ya  kujitafutia umaarufu  usio  na faida kwa  maendeleo ya uboreshaji  wa mji  huo.

Kwani  alisema  anachokifanya mbunge  huyo kutafuta  umaarufu  wa kisiasa  bila kuangalia hatari  ya kauli  zake  hizo na  kuwa  kuwahamasisha  watu  kuvunja  sheria ni kosa na kuwa  wao kama  wananchi  wanaanza  kuona kama mbunge  huyo hayupo kwa ajili ya maendeleo ya mji  wa Iringa bali kuna jambo ambalo analitafuta  zaidi ya kuwatumikia  wananchi.

'' Ni  kweli  mbunge  ndio amesababisha  leo polisi  kushindwa  kufanya  shughuli nyingine na kuja  kulala hapa kulinda amani ......ila  kesho  utamsikia  mbunge  huyo  huyo akilalamika  kuwa  kwa  nini polisi  wanatumia nguvu kubwa  kuthibitia  wananchi huku akisahau  kuwa   kauli yake  kuwataka  wananchi  kuvunja  sheria ndio imesababisha  hayo  yote''

Sanga  alitaka  wananchi  wa  jimbo  hilo la Iringa mjini  kumpima  mbunge  Msigwa  hata kwa jambo  hili la  kuwataka  wananchi  kuvunja  sheria na  kuwa  ipo  siku atawaeleza jambo jingine ambalo yawezekana  likawa  baya  zaidi  ya hili.

Obadia Kalinga  alisema  kuwa iwapo  mbunge  Msigwa  angekuwa  kweli yupo kwa ajili ya  kuwasaidia alipaswa  kukaa chini na madiwani  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  pamoja na  wafanyabiashara  hao  ili  kuwasikiliza kwanza  eneo rafiki  la  wao  kufanyia kazi  zaidi ya eneo  hilo ambalo  ni barabara ya lami ambayo imejengwa kwa kodi za  wananchi .

'' Kama  kweli anampango  wa  kuliendeleza  jimbo la Iringa mjini na anauchungu na machinga alipaswa kuwasaidia  kweli  si  kuwachezea kama hivyo  kwani ni jambo ambalo si la busara  eneo  hilo  kugeuzwa soko ni heri  hata angewaombea  uwanja  wa Mwembetogwa  ama  eneo la barabara mbili  kuliko eneo hilo''

Pia  alishauri  vyombo  vya ulinzi na usalama mkoa  wa  Iringa  kumhoji  mbunge  huyo juu ya kauli  yake  ya  kutaka  machinga hao  kurejea  eneo hilo kwani ni  sawa na kauli ya kichochezi ambayo inapaswa  kukemewa kwa nguvu  zote.

Hata  hivyo  serikali  wilayani Iringa imeutaka  uongozi  wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa kujipanga  kusimamia  sheria  zake ili kusiwepo kwa  mtu anayevunja  sheria na kuwa  zoezi  hilo la polisi  kutumika  kusimamia uvunjaji  wa  sheria  eneo  hilo si kazi ya  jeshi la polisi .

Alisema mkuu  wa wilaya  ya  Iringa Dr. Warioba  kuwa zoezi  lililofanyika leo si  zoezi  endelevu isipo kuwa Manispaa wanapaswa  kukutana na kuweka mkakati  wa  kudumu wa  kusimamia  sheria  zake.

Bila  kutaja ni zoezi  litakalofikia kikomo lini kwa  jeshi la polisi kukesha  wakilinda  eneo hilo bado mkuu  huyo  wa  wilaya  alishauri madiwani  wa Halmashauari  Manispaa ya  Iringa na mbunge  wa jimbo  hilo kukutana pamoja  ili kuweka mkakati  wa  pamoja  wa kusimamia  sheria.

Mbunge Msigwa  alitoa kauli ya  kuwaruhusu machinga  kurejea  eneo  hilo hivi karibuni katika  mkutano wa hadhara  wa  wabunge wa Chadema  waliokuwa  wamesimamishwa  bungeni na kuwataka machinga  kurejea na iwapo mtu atafika  kuwasumbua basi  wana mm!!....?