Saturday, 11 May 2013

LAMPARD AANDIKA HISTORIA MPYA CHELSEA AKIIWEZESHA TIMU KUFUZU LIGI YA MABINGWA

KIUNGO Frank Lampard ameingiza jina lake katika vitabu vya historia kwa kumpiku Bobby Tambling kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Chelsea akiifungia mabao mawili timu hiyo leo dhidi yaAston Villa.
 
Kiungo huyo wa England, aliyeanza kwenye kikosi cha kwanza kuelekea fainali ya Europa League Jumatano, kwanza aliisawazishia Chelsea dakika ya 61 kufuatia Christian Benteke kuifungia Villa bao la kuongoza dakika ya 14 kabla ya kufunga bao la ushindi na rekodi dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.
 
Sasa anatimiza mabao 203 aliyoifungia Blues, katika miaka zaidi ya 12 ya kuwepo kwake Stamford Bridge. Ushindi huo, unaifanya Chelsea ijihakikishie kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao ikiungana na Manchester City na Manchester United na sasa kazi inabaki kwa Arsenal na Spurs kuwania nafasi ya mwisho.
 
Katika mchezo huo, kikosi cha Aston Villa iliyompoteza Benteke aliyetolewa kwa kadi nyekundu, kilikuwa: Guzan, Lichaj, Vlaar, Baker, Bennett, Westwood, Delph, Sylla, Weimann, Benteke na Agbonlahor. 
 
Chelsea ambayo nayo ilimpoteza Ramires aliyepewa kadi nyekundu pia, kikosi chake kilikuwa: Cech, Azpilicueta, Cahill, Terry/Ivanovic dk75, Cole, Ramires, Lampard, Moses/Luiz dk46, Mata, Hazard, Ba/Torres dk88
 
History made: Frank Lampard strikes home from close-range to seal a precious victory - and break Bobby Tambling's 33-year record
Ameweka historia: Frank Lampard sakishangilia bao lililomfanya avunje rekodi ya Bobby Tambling ya miaka 33 ya kuwa mfungaji bora wa klabu kihistoria
 
Mobbed: Lampard is congratulated by team-mates after firing the winner
Anapongezwa na wenzake
 
Special moment: Lampard strikes his first of the game to move on to 202 Chelsea goals
Bao la 202

On target: Lampard